×

Kilichonitokea Baada ya Kubakwa na Kaka Yangu-26

Mpenzi msomaji, wiki iliyopita niliishia pale Dorcas ambaye hakujua kama alikuwa amepata ujauzito alipokuwa akijisikia ovyo huku pale nyumbani kwao akiwa amebaki yeye, Evance aliyembaka pamoja na dada mwingine. Je, kilifuatia nini? Songa mbele…

Kufuatia kutapika na kuchagua chakula nilijua nilikuwa nasumbuliwa na malaria nikawa nakunywa panadol badala ya kwenda hospitali kwa sababu nilikuwa naogopa sana kuchomwa sindano.

Ingawa mama aliposafiri alikuwa hakai muda mrefu, safari hiyo alikaa mwezi mmoja kama na wiki mbili kwani alikwenda Mwanza hadi Bukoba.

Siku aliyorejea aliponiona alinitazama na kuniuliza mbona nilikuwa nimependeza sana, nikaishia kucheka kwani sikujua alimaanisha nini, kwa kuwa alikuja na samaki wabichi aina ya sato aliniambia niwaandae kwa ajili ya kitoweo.

Kitendo cha kukumbana na harufu ya samaki, nilichafua nyongo, nilitapika sana mpaka mama akashangaa na aliniuliza nilikuwa naumwa nini, nikamwambia sikuelewa ila sikupenda tu harufu ya samaki.

Kumbe wakati huo mama alishahisi nilikuwa nina ujauzito lakini hakutaka kuniendea haraka, aliendelea kunichangamkia huku akihesabu pepsi nilizokunywa tangu alipofika ambazo zilifika nne tena za baridi sana.

Kutokana kutopenda harufu ya samaki, chakula kilipokuwa tayari sikula badala yake nilitengeneza kachumbari ambayo niliweka ndimu nyingi nikala na ugali.

Kwa jumla kila nilipolamba ndimu nilijisikia raha sana na mara kwa mara nikiwa chumbani kwangu nilikuwa nafanya hivyo na nikimaliza mabaki ya ndimu niliyatupia chini ya kitanda.

Nakumbuka ilipofika saa tisa alasiri nikiwa nimelala, mama mkubwa aliingia chumbani kwangu akaniamsha na kuniuliza nilikuwa nasumbuliwa na kitu gani, kumbe alinitega.
Kwa kuwa nilikuwa sifahamu kitu chochote nilimwambia kuna wakati sikujisikia vizuri tu na kupenda kulala, akaniangalia kwa kunikazia macho nikayakwepesha yangu.
“Dorcas!” Mama aliniita.

Nilipoitika akaniuliza kama nilianza kufanya mapenzi nikakaa kimya, akaniuliza mbona nilikaa kimya nikamwambia hata hayo mapenzi sikuyafahamu.

Baada ya kumwambia hivyo, akakunja sura na kuniambia nisijifanye mjanja kwani alikuwa anaelewa nilianza kufanya mapenzi na tayari nilikuwa mjamzito.

Aliponimbia hivyo, nilimuuliza kwa kuhamaki: “Mimi nina mimba?”
Kufuatia kumuuliza hivyo, mama aliyeona namletea mzaha alinizaba kibao ambacho kilinifanya niangukie kitandani nikaanza kulia.

“Yaani unajua kabisa una mimba, nakuuliza unajifanya hujui, sasa leo utanitambua na utanieleza huyo mbwa aliyekupatia hiyo mimba ili nikakukabidhi kwake aulee mzigo wake,” mama aliyekuwa na hasira aliniambia.

Nikiwa nalia aliniinua na kuniuliza tena kama nilikuwa nina mimba nikamwambia mama sikufahamu chochote ndipo alinihakikisha kwamba nilikuwa katika hali hiyo kwani nilikuwa nina dalili zote.

Mama aliniuliza ulikuwa ujauzito wa nani na lini nilianza mapenzi, licha ya kaka Evance kuniambia kama ningetoa siri hiyo angeniua, niliamua lolote litakalotokea katika maisha yangu litakuwa sawa kwani sikuwa na furaha ya kuendelea kuishi kwa sababu sikuwa na wazazi wala ndugu yeyote wa damu.

“Wewe kinyago si nimekuuliza nani amekupa huo ujauzito?” mama aliniuliza kwa hasira.
Huku nikiwa nalia na hasira zikiwa zimenipanda, nilimwambia mama kama kweli nilikuwa na mimba mhusika ni kaka Evance.

“Unasema mhusika ni nani?” Mama aliniuliza kwa kuhamaki.
Sikuona sababu ya kumficha, nilimsimulia kila kitu alichonifanyia, ghafla mama alinywea nikamuona machozi yanamlengalenga.

Akiwa katika hali hiyo aliniomba msamaha kwa kunipiga na kunitolea lugha kali, akanipa pole na kuniambia nilale akatoka mle chumbani na kuanza kumuita Evance.
Kumbe wakati mama ananihoji, kijana wake huyo alikuwa amesimama nje ya dirisha la chumba tulichokuwemo akisikiliza kila kitu na alipojua ambacho kingefuatia, alitoweka pale nyumbani.

Wakati mama akiendelea kumwita alitokea Emmy aliyemweleza alimuona kaka yake akielekea mitaa ya sokoni, akamuuliza alikuwa na nani akamfahamisha kwamba alikuwa peke yake.

Mama hakuwa na la kufanya akarudi tena chumbani kwangu akiwa amepoa ambapo alinikuta nimejilaza, akaniuliza kama nilihitaji kula au kunywa chochote nikamwambia soda niliyokuwa napenda kunywa, akatabasamu na kutoka mle chumbani.

Hakuchukua hata dakika moja alirejea akiwa na soda hiyo pamoja na glasi akaifungua na kuniambia nikae nianze kunywa, nikafanya hivyo naye akiwa pembeni.
Je, kilifuatia nini? Usikose wiki ijayo. Maoni, nicheki kupitia namba hiyo hapo juu.
Meneja atumbuliwa…

SASA kinachoonekana ni tumbuatumbua majipu iliyoanzishwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ dhidi ya mafisadi imeenea kila kona ya nchi, mtu akiumbuliwa katika uovu wowote, wanasema ametumbiliwa jipu na ndivyo ilivyomtokea Salim ambaye ni meneja wa usimamizi wa mafuta kwenye ‘sheli’ zilizopo mkoani Pwani.

Hussein amejitambulisha kwa kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ cha Global Publishers kuwa yeye ni mume wa Farida. Kwa hiyo Farida ni mke wake hivyo kumlalamikia Salim kuwa, alimnasa na mkewe gesti.

Hussein anadai usiku wa Desemba 15, mwaka huu alimnasa Salim akiwa na mkewe huyo tena wa ndoa kwenye gesti moja iliyopo Misugusugu, Kibaha Mkoa wa Pwani.

TWENDE PAMOJA NAYE
Akisimulia kisa chake kwa OFM ndani ya gesti hiyo majira ya saa 9 usiku, Hussein alisema yeye na Farida wanaishi Mbezi Mwisho, Dar es Salaam. Wamejaliwa kupata mtoto mmoja ambaye kwa sasa ananyonya.

Anasema: “Nilishtukia mawasiliano mabaya kati ya Salim na mke wangu. Meseji za kumchombeza mke wangu ili wakutane. Huyu jamaa namfahamu, ananifahamu, naweza kusema ni rafiki yangu. Kwa hiyo mke wangu ni kama shemeji yake. Ikaniuma sana kwani najua anaelewa mimi ni mume wa Farida.”

MKE ASHINIKIZWA
“Nilimuuliza mke wangu kwa nini ana mawasiliano hayo na Salim, akaniongopea kwamba eti meseji zilikosea namba na kuingia kwake.

“Nilimwambia kama ni kweli na ili turidhishane, wapange kukutana naye mahali kisha mimi niwashtukize kuwatokea ili aone kama Salim atajitetea sawasawa na utetezi wa mke wangu au la! Lengo kama ni kweli nimtumbue jipu kama mafisadi wanavyotumbuliwa na Magufuli siku hizi.”

SIKU YA TUKIO
Mume huyo aliendelea kuiambia OFM kuwa, siku hiyo ya tukio, mkewe na Salim walipanga kukutana saa 3 usiku kwenye baa moja iliyopo Kibaha. Baada ya kukutana wakaenda eneo linaloitwa Kibaha kwa Mathias kisha wakatoka hapo mpaka Mlandizi.

“Kote walikokuwa wanakwenda mimi na mke wangu tulikuwa tunawasiliana. Mpaka inafika saa saba usiku, wao walikuwa bado kwenye mabaa wakipata vinywaji. Nyumbani kuna mtoto ananyonya,” alisema mume huyo.

Akaendelea: “Kufika saa nane, mke wangu akasema sasa wanakuja eneo linaitwa Misugusugu ambako kuna gesti. Nilichofanya, nilimpigia simu askari mmoja kutoka Kituo cha Polisi Visiga, akaja Misugusugu.

“Alipofika, mke wangu na Salim wao walishazama chumbani muda. Ndipo tukawavamia na varangati likaibuka. Si unajua tena, mke anauma bwana. Na nyinyi mmetokea, sijui mmetoka wapi!”

OFM WALIFIKAJE?
Ilikuwa saa saba na nusu usiku, mtu mmoja alimpigia simu kamanda wa OFM na kumtonya kuhusu kuwepo kwa varangati kwenye gesti hiyo lakini hakujua ilihusu nini.
Wakati simu hiyo ikipigwa, OFM walikuwa maeneo ya Mbezi ya Kibanda cha Mkaa kuchunguza tukio moja la mfanyabiashara kudaiwa kuficha kontena eneo hilo.

Kwa kutumia pikipiki iendayo kasi, OFM waliweza kufika eneo hilo ndani ya dakika 22 kwa vile ilikuwa usiku hivyo hakukuwa na foleni kama mchana.

Nje ya gesti hiyo, OFM walikuta wananchi wenye hasira wakiwa na mishale, walioamini kuwa, varangati ndani ya gesti hiyo, huenda kulikuwa na majambazi.

Polisi aliyekutwa eneo la tukio anaitwa Romuhadi, alisema yeye aliitwa eneo hilo akiamini kuna uhalifu. Lakini kwa sababu alimkuta Hussein akimtuhumu Salim kumkuta na mke wake ndani ya gesti, ilibidi ampige pingu asikimbie ili kuimarisha usalama wa mtuhumiwa kwa vile nje kulikuwa na watu wengi, wakiwemo wahuni.

OFM KURUDI DAR, MTUHUMIWA, MTUHUMU KUELEKEA KITUONI
Saa 9 na dakika kadhaa, Salim akiwa ndani ya pingu huku akiomba msamaha mara kwa mara kwa Hussein, OFM ilishika njia kurejea Dar na afande huyo ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Visiga akiondoka na watu hao kuelekea kituoni kwa ajili ya dawati la jinsia ambalo hushughulika na matatizo kama hayo.

Leave a Comment