×

Mjengo Mpya wa Wema… Utata!

wema (1)Muonekano wa mjengo huo.

Stori: Na Musa Mateja

UTATA umegubika kuhusu umiliki wa mjengo aliohamia staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ambapo maswali yanayowasumbua wengi ni je, ameingia kwa kupanga au ameununua? Amani linakwenda sambamba na msomaji.

wema (2)TUANZIE HAPA

Hivi karibuni, Wema aliyekuwa akiishi kwenye nyumba ya kupanga iliyopo Kijitonyama ya Makumbusho jijini Dar, alidaiwa kutimuliwa na mwenye nyumba baada ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasco) kumtumbua jipu la madai ya kuchakachua huduma hizo.

wema (2)Wema Isaac Sepetu

ATII AMRI, AHAMA

Wema aliihama nyumba hiyo usiku wa Ijumaa iliyopita lakini haikujulikana mara moja anakokwenda kuishi licha ya lori lililomhamisha, aina ya Toyota Canter kuandikwa nyuma, ‘Mtu Kwao’.

wema (3)HABARI ZA JUMANNE SASA

Juzi Jumanne, chanzo kimoja kililipasha Amani kwamba Wema amehamia kwenye mjengo mkubwa na mzuri uliopo Ununio, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

“Jamani nilisoma habari kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda (ndugu na hili) la Jumatatu jana, zikisema kwamba Wema ametimuliwa kwenye ile nyumba ya Makumbusho lakini hamkusema amehamia wapi.

“Sasa mimi nawapa ubuyu. Wema amehamia hapa Ununio. Amepata nyumba nzima, kubwa. Lakini nisiwe msemaji wake mkuu, sijajua ni yake au amepanga,” kilisema chanzo hicho.

PAPARAZI WETU NYUMBANI KWA WEMA

Baada ya chanzo kuanika madai hayo, paparazi wetu alikanyaga mafuta akifuata maelezo ya chanzo mpaka kufanikiwa kufika kwenye nyumba hiyo.

wema (4)SIFA ZA NYUMBA

Ni nyumba kubwa kuliko aliyokuwa akiishi Makumbusho. Ina eneo kubwa linalokaribiakaribia ukubwa wa uwanja wa mpira. Magari makubwa matano na madogo kumi yanaweza kuegeshwa eneo la wazi la ndani.

Pia Wema anaweza kufanyia ndani kwenye uwazi huo zile sherehe zake. Na kuna madai kwamba anaandaa sherehe kubwa kwa ajili ya kuumaliza mwaka 2015 akiwa mzima wa afya njema.

PAPARAZI AZUIWA KUINGIA NDANI

Hata hivyo, paparazi wetu alipotaka kufanya utalii wa ndani, alipigwa stop na msichana mmoja aliyejitambulisha kuwa ni ndugu wa Wema pia akimhoji paparazi wetu alifikaje ndani ya ukuta wa nyumba hiyo na kusema Wema hakuwepo.

Lakini kwa macho ya haraka, paparazi wetu alibaini kuwa nyumba hiyo ina vyumba vya kulala vinne, stoo, jiko, bafu na choo kwa ajili ya jumuiya, sehemu ya kulia chakula na sebule kubwa.

AMANI LAFANYIA KAZI UTATA

Licha ya msichana huyo kumkataza paparazi wetu kuzama ndani na kujionea kwa macho yake yaliyomo, alimuuliza kama anajua Wema ni mpangaji au mmliki. “Wema amejenga hii nyumba.

We huoni kuwa ni mpya! Watu wanadhani Wema hawezi kujenga nyumba siyo! Loo! Wataisoma namba mwaka huu,” alisema msichana huyo.

PETIT MAN

Katika kuchochea utata huo, paparazi wetu alibahatika kukutana uso kwa uso na mpambe mkubwa wa Wema, Petit Man ambaye jina lake halisi ni Ahmed Hasheem na kuzungumza naye kuhusu kutolewa Makumbusho na kuhamia huko kwa sasa.

Alisema: “Tena sasa tunahamia kwenye nyumba aliyonunua Wema mwenyewe. Bonge la nyumba, mtaipata habari yake. Iko Mbezi Beach.” (Ununio huhesabika kuwa ipo Mbezi Beach).

NANI MKWELI?

Madai ya msichana aliyekutwa nyumbani, anasema Wema amejenga nyumba hiyo. Ina maana alipata kiwanja, akatafuta mafundi, wakaanza ujenzi. Madai ya Petit Man ni kwamba Wema ameinunua! Kwamba, nyumba hiyo ilijengwa na mtu mwingine, akaamua kuiuza, akanunua Wema.

WEMA HAYUPO HEWANI

Juzi, paparazi wetu alimsaka Wema kwa simu ya mkononi ili kumsikia anasemaje lakini hakuwa akipatikana hewani.

MENEJA WA WEMA

Paparazi wetu alimpigia simu meneja wa Wema, Martin Kadinda na kumuuliza kuhusu umiliki au upangaji wa nyota huyo kwenye nyumba hiyo ya Ununio.

“Kusema kweli nilisafiri, ndiyo nimerudi usiku wa jana. Muda huu najiandaa kwenda kukutana naye. Nitakuwa na majibu baadaye,” alisema Kadinda.

2 Comments

  1. M unatania ?hakuna week uyo mama amekamatwa live ameiba umeme na maji zaidi ya mwaka akatimuliwa kwenye iyo nyumba. Na wakati anahamia ikikua amenunua milioni 400.
    Nyinyi wandishi wa habari, polisi lazima mu check kama iyo nyumba sio ya wale wizi wa serikali (vigogo )wanahaha kuficha mali walizo iba. Issue iyo kali fatilieni mutapata habari. Awo wapigadebe wake wanalipwa ajili ya kutudanganya na kazi yenu kutupa ukweli lazima mu support Magufuli kusafisha inchi juu hapa ulaya ndio gumzo kubwa na sifaaa nyingi iiiii

  2. uyo mama last week alikua ametimuliwa kwenye nyumba,ameiba umeme na maji kiasi ya zaidi sh.milioni 8.na leo mnamusifu kwa nyumba mpya.
    kwa maoni yangu iyo nyumba sio ya kwake.sasa hivi vigogo wengi wanahaha kufica mali walizo iba .kutia kwa jina la wema ni chezo.wewe mwenye KUANDIKA IYI POST:
    TUNAKUOMBA KUMUSAIDIA RAIS MAGUFULI KUSAFISHA INCHI???Ungefatilia iyo issue unashirikiana na polisi mnahakikisha kama sio awo wizi wanaficha mali zao.wema hana khela ya kununua nyumba ya zaidi ya dollars 600.000na uyo petit man aache umbea atafute kazisio kushinda anadanganya umma.TUNASUBIRI KWA HAMU HABARI MPYA KUHUSU STORY YAKO.MZEE MAGUFULI NI STAR MUKUBWA APA ULAYA MUTAONA ATAFUNGUA SHULE KUFUNDISHA MA RAIS WA AFRIKA NZIMA;HONGERA SANA KWA MAGUFULI
    MWENYEZI MUNGU AMKINGE MA BA BALAA YA KILA AINA KABISA;MOISE WA AFRICA

Leave a Comment