×

Funga Mwaka Concert…. Dar Live hapatoshi leo!

new-Global-723x1024

1 Kwa mara ya kwanza kupiga kwa kutumia vyombo

2 Kutoa sapraizi ya Krismasi kwa mashabiki

3 Mshindi wa Ijumaa Sexiest Girl kujulikana

4 Watoto nao kujiachia kwa burudani kibao

KWA mara ya kwanza historia itaandikwa leo (Sikukuu ya Krismasi) ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar pale atakapotua mfalme wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na kufunga mwaka kwa kuutambulisha kwa mara ya kwanza Wimbo wa Utanipenda.

DIAMOND (3)Mfalme wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’

Akizungumza na Showbiz, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa, burudani itaanza rasmi asubuhi hii kwa watoto wote ambapo kutakuwa na michezo mingi kama vile kuteleza, kubembea, kupanda ndege maalum, kuogelea kwenye bwawa kubwa la kisasa na burudani kutoka Masai Worriors.

“Milango ya Dar Live itakuwa wazi kuanzia saa moja asubuhi ambapo watoto wote wanaruhusiwa kuja kwa kiingilio kidogo cha shilingi 2,000 na kupata burudani zote hizo hadi saa kumi na mbili jioni kisha itafunguliwa rasmi shoo ya wakubwa,” anasema Mbizo.

DIAMOND (4)Diamond

Naye Diamond alifungukia shoo ya leo akisema kuwa atahakikisha ameandika historia mpya ambayo haijawahi kutokea nchini.

“Kwanza nitatoa zawadi kwa mashabiki wangu wote watakaotoka bomba usiku wa leo ikiwa ni pamoja na kushoo love nao kwa kupiga picha na kuzungumza nao mawili matatu kabla sijapanda on stage.

“Zawadi nyingine ambayo naiona kama kubwa kwa mashabiki wangu ambao kila mwaka nafunga nao ndani ya Dar Live ni ya kupiga shoo ya live kwa kutumia vyombo nikiwa na timu yangu nzima ya Wasafi Classic Baby (WCB) na siyo wa kukodi kama wafanyavyo wengine.

“Mashabiki watarajie kuzisikia nyimbo zangu zote live kama vile Mbagala, Mdogomdogo, Nasema Nawe, Nana, Nitarejea, Nataka Kulewa, Kesho, Moyo Wangu bila kusahau huu ambao ni habari nyingine ya mjini wa Utanipenda,” anasema Diamond.

c7Msaga Sumu

Mbali na Diamond, usiku huo utapendezeshwa pia na bingwa wa muziki wa Singeli, Msaga Sumu ambaye atapiga shoo mwanzo mwisho kuhakikisha mashabiki wote wa muziki huo wa ‘kiswazi’ wanapata burudani waitakayo.

“Siku zote nikiwa Dar Live huwa sikosei, nitapiga ngoma zote kuanzia Shemeji Unanitega, Huyu Mtoto, Inaniuma Sana, Naipenda Simba na nyingine nyingi,” anasema Msaga Sumu.

wakliWakali Dancers

Kuonesha kuwa Krismasi inakwenda vizuri, mashabiki pia wategemee kuliona kundi linalobamba Afrika Mashariki kunako miondoko ya kucheza, Wakali Dancers wakikamua jukwaani.

Wakali Dancers watahakikisha wanakamua ngoma zote za kijanja za ‘town’ jukwaani kwa mastaili kibao ambayo hayajawahi kufanyika.

Fainali Ijumaa Sexiest Girl

ikmmmVanessa Mdee ‘Vee Money’.

Kuonesha kuwa burudani zitakuwa za kumwaga, kwa wale wafuatiliaji wa lile shindano la msanii mwenye mvuto linaloendesha na gazeti hili (Ijumaa Sexiest Girl 2015) kwa mara nyingine watapata fursa ya kumjua mshindi.

luluElizabeth Michael ‘Lulu’

Shindano hili ambalo limedhaminiwa na Hamadombe Distributor hadi sasa limebakiwa na washiriki watatu walioingia fainali ambao ni Asha Salum ‘Kidoa’ Elizabeth Michael ‘Lulu’ pamoja na Vanessa Mdee ‘Vee Money’.

AshaSalumKidoaAsha Salum ‘Kidoa’

Miongoni mwa zawadi atakazoibuka nazo mshindi wa shindano hili ni pesa taslim, tuzo, cheti, ofa ya bure ya kufanya shopping ya nguo na kutengenezwa nywele kwa kipindi cha miezi sita kwenye saluni ya Bulldozer iliyopo Kigamboni jijini Dar.

Mtonyo sasa!

Burudani yote hiyo itakuwa ni kwa kiingilio cha Sh. 15,000 (kawaida) na kwa V.I.P ni Sh. 30,000 tu.

Mbali na kiwango hicho, wadhamini wakuu wa shoo hii ambao ni Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi Airtel, kupitia huduma yao ya kijanja kimawasiliano ya Airtel Money Tap Tap watatoa punguzo la kiingilio kwa tiketi 1,000 endapo utakata kwa kutumia huduma hiyo mpya.

Unachopaswa ni kuwa na kadi yako ya Airtel Money Tap Tap inayopatikana kwa mawakala wote wa Airtel waliopo Temeke na Ilala na ukifika nayo Dar Live utapata punguzo la Sh. 5,000 yaani tiketi ya Sh. 15,000 utapata kwa Sh. 10,000 na ya Sh. 30,000 itakuwa Sh. 25,000.

Leave a Comment