×

Pluijm: Mchezaji bora alikuwa Kaseja

pluijmKocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm.

Nicodemus Jonas,Dar es Salaam
PAMOJA na kuruhusu mabao matatu katika kichapo cha mabao 3-0 walichopokea Mbeya City mbele ya Yanga, juzi Jumamosi, bado Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amemtaja kipa wa Mbeya City, Juma Kaseja kama mchezaji bora katika mchezo huo kwa kile alichosema aliiokoa timu hiyo kwa mengi.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Kaseja ambaye aliwahi kukipiga Yanga, alifanya kazi ya ziada kuiokoa Mbeya City lakini mashambulizi ya kila mara kutoka kwa Amissi Tambwe, Deus Kaseke na Donald Ngoma yakamzidia dakika ya 35 baada ya Tambwe kumtungua.

Katika takwimu, Kaseja alichomoa michomo hatari minne, ukiwemo wa Kaseke, Thaban Kamusoko mara mbili na Tambwe, huku akimaliza mchezo akitoa ‘saves’ 14.

Akizungumzia wapinzani wake, Pluijm alisema: “Walicheza kama nilivyotarajia, mpira wao ni nguvunguvu tu, nafikiri kwa kuwa wanafundishwa na mwanajeshi. Kaseja alikuwa kwenye ubora wake, alifanya kazi kubwa na ukweli aliwaokoa sana. Alifanya ‘savings’ nyingi hatari ambazo pengine matokeo yangekuwa zaidi ya haya.”

Leave a Comment