×

Rigwaride la afande -10

ILIPOISHIA RISASI JUMAMOSI:
Wote tulipitiwa na usingizi, tena ule wa fofofo. Mimi nililala kama nipo kitandani kwangu nyumbani maana nilijiachia. Mimi nikilala huwa sibakizi nguo yoyote zaidi ya kujitupia shuka tena nusu mwili, usiku sana kama kutakuwa na kijibaridi.

Wote tulishtuliwa na sauti ya ukali ya mama akiita kwenye mlango wa chumba cha afande Mwita…
“We Rhoda…” huku akigonga mlango kwa nguvu…
JIACHIE NAYO MWENYEWE SASA…

“Mm! Mama amerudi tena,” nilisema kwa kumnong’oneza sikioni afande Mwita…
“Naamini hakwenda. Alikuwa nje akifuatilia…”
“Sasa amejuaje mimi nimo ndani? Maana ameita kama ana uhakika wakati ulishamwambia niliondoka muda uleule.”

“Kwanza ameingiaje ndani, mlango nilifunga,” alisema afande Mwita.
Alitoka kitandani, akaenda hadi mlangoni na kuanza kuongea na mama…
“We mama…”

“Mimi namtaka binti yangu tu.”
“Si nilikwambia aliondoka!”
“Sijaamini…mbona nilisikilizia dirishani nikasikia kitanda kikilalamika kwa muda mrefu, uko na nani kwani?”

“Sasa mama hapo utakuwa unaingilia uhuru wangu binafsi. Yaani kitanda changu kulia wewe inakusumbua nini? Unapotaka kujua niko na nani ili iweje?”
Ghafla nilimsikia mama akitembea kutoka nje huku akinilaani kwa maneno makali kabisa…

“Mtoto hasikii, amekuwa kama hana baba wala mama. Yeye kulala kwa wanaume haoni tabu. Ananiumiza sana huyu mtoto.”
Nilinyamaza kimya, hata dalili ya kukohoa iliponijia, nilijiminya sana.
Akiwa anapita usawa wa dirisha, nikamsikia akisema…
“Na mimi hapa leo sitoki mpaka nimwone huyo mwanaume aliyemchukua binti yangu. hata akirudi saa kumi na moja, atanikuta tu.”

Kauli hiyo ilinitisha sana, niliogopa. Sasa mama aliamua kupambana na mimi na afande Mwita, eti hataondoka kurudi nyumbani.
Simu yangu niliitoa mlio mapema sana ili kukwepa kuumbuka ikipigwa…
“Unamsikia mama yako anavyosema?” aliniuliza afande Mwita…

“Namsikia, sasa itakuaje? Atakaa kweli, mimi namjua mama yangu, akisema amesema, hatoki huyu mpaka usiku umkute hapahapa,” nilimwambia afande Mwita.
“Ataondoka tu, akibisha nitamwitia mwizi, sitanii hata kidogo,” alisema afande Mwita.
Ghafla, nilimsikia afande Mwita akishtuka na kusema…
“Ohooo..!”

“Vipi tena?” nilimuuliza na mimi nikiwa nimeshtuka…
“Sikia hapo nje,” alisema, nikatega sikio vizuri.
Nilijua mama anaendelea kuongea, lakini nilichokisikia, kilinishtua sana…
“…kwa hiyo wewe mama umekuja kumfuata huyo binti yako?”
“Ndiyo…sasa kuna mtu kasema huyo mwanaume kaenda kwenye lindo, sijui ni askari. Akasema atarudi saa tisa usiku. Nikaondoka, nikamwacha binti hapa, baadaye kurudi naambiwa eti nilipoondoka na yeye akaondoka,” alisema mama.

Sauti ya kiume iliyokuwa ikihoji niliihisi kama ni ya afande Mwira…
“Mama mimi sijui lolote. Mimi ndiyo afande Mwira mwenyewe na kweli nilikwenda kwenye lindo na bado nipo kwenye lindo, nimerudi kwa dharura tu,” alisema huyo mwanaume ambaye mwenyewe alijiweka wazi kwamba ni afande Mwira…
“Kimenuka,” nilimwambia afande Mwita…

“Tulia wewe,” alinitia moyo wa ujasiri…
“Lakini baba mimi kwa akili zangu naamini binti yangu hakuondoka, yupo humuhumu ndani.”

“Mh! Mama una uhakika? Ndani atakuwa kwa nani sasa?”
“Yule mwanaume aliyetujibu mmekwenda lindo si yupo?”
“Kwa hiyo atakuwa ndani kwake?”
“Naamini.”

“Ngoja nikakuangalizie,” alisikika akisema afande Mwira…
“Anakuja,” nilisema.
“Tulia wewe…nimeshakwambia tulia. Mbona hutulii?”
Nilitulia kama maji kwenye jagi. Lakini mapigo ya moyo yalikuwa yakinienda kwa kasi ya ajabu.

Viatu vya afande Mwira vilisikika vikipita dirishani. Inavyoonekana, wenyeji wa nyumba hiyo wanatumia mlango wa nyuma kuingia ndani na si mlango mkubwa wa mbele.
Lakini mimi niliingizwa kwa mlango mkubwa japokuwa niliondoka kwa kupitia dirishani.

Mara, mlango wa uani ukafunguliwa, viatu vikatembea tena mpaka mlangoni kwa afande Mwita…
“Afande Mwita,” aliita huku akigonga mlango kwa ustaarabu kidogo.
“Afande Mwira…”
“Vipi za kazi bwana?”

“Njema. Nimerudi.”
“Oke. Na mimi nimefuata simu yangu niliisahau. Kuna mama hapo nje anamtafuta binti yake anaitwa Rhoda, unamjua?”

“Huyo mama nimeshamjibu, alipoondoka yeye na binti yake aliondoka. Sasa sijui anataka nimwingize hadi chumbani akague au vipi?” afande Mwita alimjibu mwenzake huku mkono wake mmoja ukitua kwenye ncha ya nido langu moja, nikashtuka na kutoa kaukelele kidogo maana nilisisimka mwili mzima. Na mimi sehemu yangu ya kuchanganyikiwa ni hiyo.

“He! Kuna nini tena?” aliuliza afande Mwira, maana yake alisikia ule ukelele wangu…
“Hakuna kitu…ye aende zake tu bwana…”
“We baba wewe…unasema binti yangu aliondoka muda uleule wakati nimemsikia sasa hivi ameshtuka hapo, sijui umemtekenya!” alisema mama ikionekana na yeye yupo mlangoni.

Afande Mwita badala ya kujibu, akajisahau na kunishika tena, safari hii nikasema kwa sauti kabisa…
“Bwana nini?”
Je, nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Risasi Jumamosi ijayo.

Leave a Comment