×

Talaka feki yawarudisha watoto nyumbani

WAKATI Wakristo duniani kote wakijiandaa na Sikukuu ya Krismasi, watoto wa familia moja Kisesa, Mwanza, wamejikuta wakiikaribisha sikukuu hiyo kwa staili ya pekee baada ya kupokea taarifa za uongo kutoka kwa baba yao zilizodai kuwa anamtwanga talaka mama yao.

Chanzo chetu kilisema kuwa baba huyo alifikia hatua hiyo kutokana na watoto wake wanaoishi nchi za nje kutorudi nyumbani kwa wazazi wao kwa takriban miaka sita tangu walipoondoka jambo lililowafanya wazazi hao wabuni uongo huo wakijifanya wanatalikiana ambapo baada ya kusikia taarifa hizo watoto hao walipigiana simu na kupeana habari hiyo mbaya na kukubaliana kurudi nyumbani haraka.

“Unaambiwa ile wanafika wakijua wanakuja kuwasuluhisha, wakapokewa na wazazi wao kwa furaha na kuwaambia waandae sikukuu jambo lililowafanya wakasirike lakini baadaye wakaelewa hivyo nyumba yao kutawaliwa na furaha,” alisema mdaku wetu.

Leave a Comment