×

Dairekta awapa makavu mastaa

Mwandishi wetu
DAIREKTA wa sinema aliyeiongoza sinema ya Paulo na Sila, Baraka Chigele ameibuka na kusema anawashangaa mastaa wakubwa wasioamini katika sura mpya kila siku pasipo kujua wanadidimiza soko la filamu.

Akizungumza na mwanahabari wetu, Chigele alisema mastaa wengi wa filamu ambao wana kampuni zao za kuzalisha filamu, wamekuwa wakishindwa kusogea mbele kwa kuendekeza kuwachezesha mastaa wenye majina kila uchwao wakati kuna vipaji vingi.

“Ndiyo maana mimi katika sinema ya Paulo na Sila, wamecheza watu wageni kama Emmanuel Gukwi na Shangwe Roti ambao wameonesha uwezo mkubwa na filamu imekuwa kali, mashabiki wataiona siku siyo nyingi inaingia mtaani,” alisema Chegele.

Leave a Comment