×

Rigwaride Ra Afande

ILIPOISHIA RISASI JUMATANO:

“We baba wewe…unasema binti yangu aliondoka muda uleule wakati nimemsikia sasa hivi ameshtuka hapo, sijui umemtekenya!” alisema mama ikionekana na yeye yupo mlangoni.

Afande Mwita badala ya kujibu, akajisahau na kunishika tena, safari hii nikasema kwa sauti kabisa…
“Bwana nini?”

SHUKA NAYO MWENYEWE…

Nilishtuka sana mwenyewe kubaini kuwa, nimesema kwa sauti. Nikamwona afande Mwita akiniambia shiii!
“Ah! Haya sasa, mambo yote tayari sasa…tunasubiri nini?” alisema mama akiashiria kwamba, amenisikia…

“Rhoda hakuna jinsi, itabidi nifungue mlango tu utoke, mama yako ameshasikia kila kitu,” aliniambia afande Mwita kwa sauti ya chini. Uso wake ulijaa wasiwasi na mshangao mkubwa.

Niligeuka kuangalia dirisha, nikabaini ni kama la kwa yule afande wa muda ule. Lilikuwa dirisha kubwa, lakini halikuwa na nondo…
“Kwani siwezi kutokea dirishani?” nilimuuliza.

“Afande mwita ungekuja na huyo binti, mama yake ameshamsikia,” alisema afande Mwira huku sauti yake ikimalizikia kuonesha anaingia chumbani kwake. Bila kupoteza muda, nilipanda kwenye lile dirisha ili nirukie nje, afande Mwita akanishika mguu kunizuia…

“Ukiumia je?” aliniambia kwa sauti huku amenitumbulia macho.
Sasa akiwa bado amenishika mkono, alifungua mlango ili tutoke na tuonekane na mama.

Mama ile kuniona tu akanivaa, tukaenda wote mpaka chini…
“Mama unaniua…”

“Na mimi lengo langu ufe, malaya mkubwa wewe. Sasa huyu ndiye nani? Kwa nini ulin’tajia mtu mwingine wakati anayehusika ni huyu,” alisema mama kwa sauti ya juu, nikajua nje ‘nzi’ watajazana sasa hivi…

“Mama hata mimi siye ninayehusika, shetani tu ametupitia mimi na yeye. Mtu wake ni huyu afande uliyeingia naye ndani…”

“Wewe baba wewe…acha uongo wako. Hauna maana. Mimi ni mtu mzima, najua kila kitu. Wewe ndiye nimekunasa na mwanangu, lazima utamuoa,” mama alisema akiendelea kunishushia kipondo cha nguvu.

Ikabidi afande Mwita aingilie kwa nguvu, kiaskari sasa ili kuniokoa. Ikawa ndiyo salama yangu…

“Mama ukiendelea kumpiga huyu binti hatua kali za kisheria zitafuata juu yako,” alisema afande Mwita.
“Mimi ninachojua baba, huyu binti kuanzia sasa anaishi kwako na ni mkeo. Kula, kunywa, kulala mpaka matibabu ni juu yako, kwa heri Rhoda,” alisema mama na palepale kuondoka zake huku akitembea kwa hasira.

Nilibaki chini huku nikiendelea kulia kidogokidogo, kilio changu kikisindikizwa na kwikwi kwa mbali huku mkono mmoja nikiufunika uso…

“Ingia ndani sasa,” afande Mwita aliniamuru, nikasimama na kuingia ndani kwake.
Nilifikia kwenye kitanda na ndiyo nikaacha kulia na kuangaliana na afande Mwita.
Nasema kuangaliana kwa sababu wakati namwangalia, nilibaini na yeye ananiangalia. Kwa hiyo ni sahihi kabisa nikesema tulikuwa tunaangaliana. Nilimlegezea macho, yeye akanikazia na kusema…

“Ndiyo umeshakuwa mke wangu sasa.”
Kwa mara ya kwanza nilijikuta nikitabasamu…
“Unatabasamu mazuri hayo?” alinijia juu…

“Jamani sasa nilie…mama kanikuta kwako, nimekwambia nitokee dirishani ukanikatalia. Nikisema ulitaka mwenyewe kuozwa kwa nguvu nitakuwa nakosea?”
“Utakuwa unakosea sana. Wewe ndiyo ulitaka ujulikane uko kwangu. Ni nini kilikufanya useme kwa sauti muda ule?”

Wote tukawa kimya, mimi mwili ulishalegea kwa kipigo cha mama. Japo kwa muda mfupi lakini nilichoka sana.

Tukiwa chumbani, tulimsikia afande Mwira akija mlangoni kwa afande Mwita…
“Afande,” aliita kwa sauti ambayo hakupenda kurudia tena kuita kwamba, afande Mwita hakusikia…
“Ee afande.”

Kulipita ukimya wa sekunde kama tano, afande Mwira hakusema njoo wala lolote lingine, afande Mwita akajua shida yake aende. Alifungua mlango, akasimama katikati…
“Ee bwana pole sana. Lakini ndivyo maisha yalivyo. Sasa utafanyaje?”

“Ndiyo niko naye hapa binti,” alisema afande Mwita huku akigeuka na kuniangalia nilipokuwa kwenye kitanda kisha akaufungua mlango kidogo ili afande Mwira anione, nikaachia tabasamu baada ya kukutana macho na afande Mwira, ‘nikakumbuka mbali’.
“Hujambo binti?”

“Sijambo, shikamoo.”
“Marhaba…pole sana…”
“Asante,” niliitikia nikiwa najificha uso.
“Au afande Mwita ungemwambia aende kwa ndugu yake yeyote kama anaye hapa Temeke,” alisema afande Mwira…

“Akha! Mi sina ndugu hapa Dar,” nilidakia mwenyewe tena si kwa kusema Temeke tu, Dar nzima.

“Lo! Imekula kwako afande Mwita…sasa lakini wewe binti naye, ikawaje mpaka ukakubali kumleta mama yako hapa nyumbani?” alisema afande Mwira. Kabla hajajibu, afande Mwita akasema anakwenda chooni mara moja. Afande Mwira akabaki amesimama mlangoni…

“Kwanza utakuwa mke wa nani humu ndani sasa?” aliniuliza kwa sauti ya chini, nikatabasamu…
“Wewe hapo,” nilisema kwa sauti ya chini. Akanifuata kitandani haraka sana, akanipa denda, nikalipokea bwana…
Je, nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kweli Risasi Jumatano ijayo.

Leave a Comment