DADA wa aliyekuwa mfalme wa muziki wa Pop, marehemu Michael Jackson, Janet Jackson ameamua kuzima tetesi zilizokuwa zinaendelea kuzagaa juu ya afya yake kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya koo.
Jana jioni (Jumatano), Janet aliamua kuanika wazi kupitia wimbo aliouchia ghafla uitwao The Great Forever ambapo ndani yake kuna mistari anayosema ‘muache kutengeneza ukweli muutakao.’
‘Kumbuka… amini kile ninachokiongea kwa mdomo wangu.’
Licha ya kuachia wimbo huo, aliposti pia kipande cha video ya wimbo huo na kuandika maneno yaliyosomeka;
“Tetesi hazina ukweli. Sina kansa. Ni mzima.”
Akaongeza; “Dokta wangu amenihakikishia kuwa ratiba yangu ya tamasha la Ulaya itaendelea kama kawaida, huko kuahirishwa hakuko kwenye ratiba.”
Hivi karibuni, tetesi zilizagaa kuwa Janet amepatwa na kansa ya koo hivyo hataweza kuendelea na ziara yake kubwa barani ulaya aliyoiita jina la Unbreakable Tour.
(Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL)
