Mwandishi Wetu
MSANII wa Bongo Fleva, Andrew John ‘Sanjay Boy’ amefunguka kuwa anajivunia kufanya kazi na msanii anayefanya muziki pande za Marekani aitwaye MK Kingson.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Sanjay Boy alisema alikutana na Mmarekani huyo ambaye pia anamiliki studio nchini humo alipokuja hivi karibuni kwenye ziara binafsi ndipo alipokutana naye wakazungumza na kuona amshirikishe.
“Jamaa ni msanii mzuri, nilipomueleza kuhusu kolabo akakubali. Tukaingia Mazuu Records, tukarekodi wimbo wangu wa Baby, kazi itatoka wiki ijayo redioni,” alisema Sanjay.