×

Ascaris; Minyoo inayosumbua wengi-2

Ascaris-male-and-female_1-13a9fthWiki iliyopita katika makala haya tuliishia kipengele cha athari za minyoo jamii ya Ascaris. Leo tunaendelea na sehemu ya mwisho ya kipengele kinachofuatia hapo chini ili msomaji apate elimu kuhusu  ugonjwa huo, kinga na tiba yake, endelea:

Kadiri mabuu yanavyosafiri sehemu mbalimbali za mwili, wanaweza kusababisha uharibifu wa viungo vya ndani, kuvimba tumbo na kuvimba ini au wengu, kusababisha sumu mwilini na kichomi.

Ascaris_lumbricoides_adult_wormsMtu hupata minyoo kwa kula mayai kutoka kwenye udongo uliochanganyika na kinyesi cha binadamu au mboga na maji ni njia ya msingi ya maambukizi.

Uhusiano wa karibu na wanyama wanaofugwa majumbani walioambukizwa na udongo wenye vimelea, unaweza kusababisha maambukizi.

Maambukizi pia hutokea kwa njia ya maji machafu kutumika kwenye mashamba na mbogamboga hizo kusafirishwa huku zikiwa zimechafuliwa na vimelea vya minyoo.

Maambukizi kutoka kwa binadamu kwenda binadamu mwingine huwa haitokei. Mtu anaweza kugundulika kuwa ana minyoo kwa kupimwa kinyesi au matapishi yake kwani vimelea vya ova vinaweza kuonesha mayai au minyoo.

Kinga

Jamii itumie vyoo, ulinzi wa chakula ufanyike, kisigusane na chochote chenye vimelea vya minyoo na watu wahakikishe wananawa mikono kabla ya kula, matunda pia yaoshwe kabla ya kuliwa. Watoto wasiruhusiwe kula chakula kilichoangushwa chini bila kuoshwa au kupikwa.

Tiba

Zipo dawa nyingi zinazotumika kuua Nematode ambao ni minyoo kama vile Mebendazole ambayo huua minyoo polepole, Piperazine husababisha au huzuia kusambaa kwa minyoo wakati tiba inapofanya kazi kwa kutumia dawa zisizo na nguvu sana, Pyrantel Pamoate,  Depolarizes, Albendazole, Thiabendazole, Hexylres.

Leave a Comment