×

Ugonjwa wa kisukari unavyosumbua wengi

kisukari

Ugonjwa wa kisukari kitaalam huitwa Diabetes Mellitus unasumbua watu wengi duniani na hutokea pale tezi kongosho au Pancrease inaposhindwa kutengeneza homoni au kichocheo aina ya Insulin.

Ugonjwa huu ni kati ya magonjwa yasiyoambukiza, wengine hupata ugonjwa huo pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho cha Insulin na kusababisha kuongezeka kiwango cha sukari kwenye damu au kitaalam Hyperglycemia.
Insulin ni kichocheo au homoni inayotengenezwa na kongosho ili kudhibiti sukari katika damu mwilini.

Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababishwa na mtu kuwa na kiwango kidogo cha Insulin mwilini, mwili kutosikia kichocheo hicho au yote mawili.

Ili kuelewa vyema ugonjwa wa kisukari ni muhimu kwanza kuelewa namna chakula kinavyovunjwavunjwa na kutumiwa na mwili ili kuzalisha nguvu.

Wakati chakula kinapoyeyushwa matukio kadhaa hutokea. Moja ni sukari inayoitwa Glucose ambayo ni chanzo cha nguvu mwilini huingia katika damu.
Tukio la pili ni kiungo kinachoitwa kongosho au kwa kimombo Pancrease kutengeneza kichocheo cha Insulin.

Kazi ya Insulin ni kuondoa Glucose katika damu na kuingiza katika misuli, seli za mafuta na ini, ambako hutumiwa kama nishati.

Watu wenye ugonjwa wa kisukari huwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kwa sababu miili yao haiwezi kupeleka sukari kwenye seli za mafuta, ini na misuli ili ihifadhiwe kwa ajili ya kuzalisha nguvu.

Hii ni kutokana na moja ya sababu zifuatazo. Huenda kongosho zao haziwezi kutengeneza Insulin ya kutosha au seli za mwili wao haziathiriwi na Insulin kama inavyotakiwa au sababu zote hizo mbili.

Saratani
Kuna saratani au kansa aina nyingi kwa mfano. Saratani ya tezi ya Thyroid. Hii ni aina ya saratani inayokumba tezi ya Thyroid. Ikumbukwe kuwa tezi ya Thyroid ipo sehemu ya mbele ya shingo ya mwanadamu ikiwa na sehemu mbili Lobes moja kila upande wa shingo.

Dalili hutofautiana kulingana na aina ya saratani, ingawa kiujumla zaweza kujumuisha.

Saratani ya Damu:
Leukemia ni saratani inayoshambulia tishu za mwili zinazohusika na utengenezaji wa damu zikiwemo supu ya mifupa Bone Marrow na mfumo wa Lymph Lyphatic System. Kwa maneno rahisi, Leukemia humaanisha saratani ya damu. Kuna aina mbalimbali za Leukemia, nyingine zikiathiri watoto na nyingine zikiathiri zaidi watu wazima.

Kansa ya Mfuko wa Uzazi:
Kansa ya mfuko wa kizazi huwapata akina mama ambao wameshafikia ukomo wa kupata hedhi kila mwezi na ambao wana umri kati ya miaka 55 hadi 69. Aidha, wanawake wanakuwa katika hatari kubwa zaidi iwapo kiwango cha homoni aina ya Oestrogen kitakuwa juu kuliko kawaida.

Wanawake wanene Obese nao wapo kwenye hatari ya kupata aina hii ya kansa kwa vile wengi wao huwa na kiwango cha juu sana cha homoni hii ya Oestrogen kwa vile mafuta yaliyorundikana mwilini hubadilisha homoni za aina nyingine kuwa Oestrogen.

Saratani ya Matiti:
Saratani ya matiti hutokea kwenye titi ambalo kwa kawaida lina sehemu ya kutengeneza maziwa ijulikanayo kama Lobules na aina fulani ya mishipa inayounganisha hizi Lobules na chuchu za titi.
Itaendelea wiki ijayo.

Leave a Comment