×

SSRA kutumia mfumo wa kielekroniki kupokea malalamiko

1. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utafiti ,Tathimini na Sera, Ansgar Mushi, Ofisa wa Tehama, Ernest Masaka,na Ofisa Uhusiano, Agnes Lubuva.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utafiti ,Tathimini na Sera, Ansgar Mushi, Ofisa wa Tehama, Ernest Masaka na Ofisa Uhusiano, Agnes Lubuva.2.Viongozi hao wakisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari (hawapo pichani).

Viongozi hao wakisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari (hawapo pichani).

3.Wanahabari wakichukua tukio hilo.

Wanahabari wakichukua tukio hilo.

MAMLAKA  ya Usimamizi na udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) imeanzisha utaratibu mpya wa kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama kwa kutumia mfumo wa kisasa wa kielekroniki (Tehama).

Akizungumza na wanahabari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), Ofisa wa Mfumo wa Tehama, Ernest Masaka amesema kwa sasa mwanachama yeyote mwenye malalamiko kuhusu huduma za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii au maoni mbalimbli anaweza kufanya mawasiliano na mamlaka kwa urahisi kupitia njia ya kielektroniki (Mobile App) inayopatikana kwa watumiaji wa simu za mkononi.

Amesema mtu anaweza kuipata huduma hiyo kwa kupata msaada wa malalamiko au maoni kwa kwenda kwenye simu yake ya mkononi ‘Google Play’ kupitia jina la SSRA au kupitia tovuti ya mamlaka ya www.ssra.go.tz kisha  ataona sehemu iliyoandikwa malalamiko au maoni na kuelezea shida yake.

Masaka ameeleza kuwa uanzishwaji wa mfumo huo ni moja ya hatua mbalimbali ambazo zimekuwa zikichukuliwa na mamlaka katika kulinda na kutetea maslahi ya wanachama, akisema ni kwa mujibu wa sheria ya mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii namba 8 ya mwaka 2008 iliyoboreshwa kwa sheria namba 5 ya mwaka 2012.

Aidha utaratibu huo umeanzishwa ili kumrahisishia mwanachama au mwananchi kutoa malalamiko yake kuhusu masuala ya sekta ya hifadhi ya jamii au maoni ya kuboresha sekta hiyo ambapo mtu anaweza kufanya hivyo akiwa mahali popote na kwa muda wowote.

Hata hivyo Masaka aliongeza kuwa mara tu mwanachama au mtu atakapokuwa tayari ameingiza taarifa zake katika mfumo huo wa kielektroniki kama vile jina la kwanza, kati na la ukoo, anuani na namba ya simu mfumo huo hutoa namba ya kumbukumbu kwa mlalamikaji au mtoa maoni ili taarifa hizo zimtambue kuweza kupata mawasiliano namna ya kumsaidia pamoja na kuufanyia kazi ufuatiliaji wa tatizo husika.

Na Denis Mtima/Gpl

Leave a Comment