CATARINA, ambaye alikuwa ameweka nadhiri kwamba mwanaume atakayemtoa bikira yake ni Kevin, tayari ameshaingiliwa kimwili bila kupenda akiwa Afrika Kusini. Usiku yeye pamoja na meneja wake Craig wakiwa kwenye onyesho la mwanamuziki kutoka Marekani, Barbara Johnson, Catarina anashawishiwa kunywa mvinyo ambao Craig aliuchanganya na pombe kali wakati mrembo huyo alipokwenda msalani, analewa na kupoteza fahamu, asubuhi anaamka na kukuta amelala kwingine halafu shuka lina damu, kujiangalia anakuta ameshatolewa bikira halafu anashtuka kuona bilionea aliyekuwa anamhusudu, Jackson Motown anatoka bafuni kuoga huku akicheka. Analia kwa uchungu. Je nini kitaendelea?
SONGA NAYO…
CATARINA alilia mno, hakukumbuka kulia hivyo maishani mwake! Jackson Motown alikuwa amesimama mbele yake, alimwona kama mzimu, mikono kiunoni! Maneno yake ya kujidai aliyoyasema siku nyingi kabla; ipo siku utakuja kuwa mke wangu…yalijirudia kichwani kwa Catarina ambaye hasira ilizidi kumpanda.
Hasira hiyo haikuwa dhidi ya Motown peke yake bali pia Craig Anderson, alikuwa na uhakika kabisa kilichotokea ulikuwa ni mchoro, Craig alimnywesha pombe kwa makusudi ili alewe na baadaye kumpeleka chumbani kwa Motown ambako alibakwa kinyama, roho ilimuuma mno, hasa alipomfikiria Kevin na bikira aliyoipoteza, zawadi pekee aliyoitunza kwa ajili ya mume wake mtarajiwa.
“Why have you done this to me?”(Kwa nini umenitenda hivi?)
“I love you Catarina, I want you to be my wife.”(Nakupenda Catarina, nataka uwe mke wangu!)
“You can’t rape someone you love!”(Huwezi kumbaka mtu unayempenda!)
“There was no option!”(Hapakuwa na njia nyingine!)
“This is the crime, I am going to report it to the police!”(Hili ni kosa la jinai, nitakwenda kutoa taarifa polisi!)
“Do you think you will have any justice?”(Unafikiri utapata haki yoyote?)
“I will make sure you go to jail!”(Nitahakikisha umefungwa!)
“Me? Go to jail? Go ahead!”(Mimi? Nifungwe? Nenda!) aliongea Motown kwa kujidai.
“You are an animal, you don’t deserve to live!”(Wewe ni mnyama, hutakiwi kuishi!) aliongea Catarina akijifuta machozi, ubongoni mwake taswira ilikuwa ni ya Kevin tu, alijiona mjinga kwa kukubali kunywa pombe, hakuwa na maneno ya kumweleza Kevin ili aweze kumwelewa, mwisho kabisa alifikiria hali yake ya afya, pengine alikuwa ameambukizwa virusi vya Ukimwi.
“Did you use condom?”(Ulitumia mpira?)
“It feels no sweet in a condom!”(Huwa sisikii raha nikitumia mpira!)
“F…” Catarina alitaka kutamka neno lakini akashindwa, hasira ilikuwa imemshika, alitamani apate kisu na kumchoma nacho Motown.
Ghafla mlango ukafunguliwa, Craig akaingia na kwenda moja kwa moja kupiga magoti mbele ya Catarina aliyekuwa bado akilia na kuanza kumwomba msahama kwa yote yaliyotokea akimuahidi malipo makubwa ya fedha kutoka kwa Motown, Catarina hakuweza kuongea chochote, kooni alikuwa amekabwa na kwikwi ya hasira.
“Forgive me!”(Nisamehe!)
“Why do this to me?”(Kwa nini umenifanya hivi?)
“I am sorry!”(Samahani!)
“So you brought me here to be a sex slave?”(Kwa hiyo ulinileta hapa kuwa mtumwa wa ngono?)
“No!”(Hapana!)
“You sold me to your client!”(Uliniuza kwa mteja wako!)
“Forget about what happened! This is how the Modeling world works, about every model does this! Some sell themselves on Instagram by posting nude photos, then men call and pay lots of money to have sex with them”(Sahau yaliyotokea, huu ndiyo ulimwengu wa mitindo, kila mwanamitindo hufanya hivi, wengine hujiuza wenyewe kupitia Mtandao wa Instagram ambako huweka picha zao za kuvutia na wanaume huwapigia simu na kuwalipa fedha nyingi ili wafanye nao ngono!)
“I am not such a kind of girl, for sure I am going to report this to the police!”(Mimi sio msichana wa aina hiyo, hakika ninakwenda kutoa taarifa polisi!)
“Oh my God! If you dare do that, your Modeling contract will be terminated instantly!(Mungu wangu! Ukithubutu kufanya hivyo, mkataba wako utasitishwa mara moja!)
“I don’t care as long as you two will go to jail!”(Sijali ili mradi mtakwenda jela!)
“Fighting with me is like hitting your fist to wall!”(Kupigana na mimi ni kama kupiga ngumi ukutani!) aliongea Motown.
“Take me to my Apartment!”(Nipeleke nyumbani kwangu!)
Craig alimshuhudia Catarina akivaa na baadaye alipomaliza walishuka hadi chini na kuingia kwenye gari, njia nzima pamoja na kitisho alichotoa Craig alikuwa akiendelea kumbembeleza Catarina asichukue hatua aliyoahidi, walipofika nyumbani kwake, bila kuongea chochote Catarina alishuka na kubamiza mlango kisha kupandisha juu ambako alijifungia na kuanza kulia.
Alifikiria jinsi ya kuwaeleza wazazi wake na Kevin juu ya kilichotokea hakupata maneno, kwani kitendo cha yeye kunywa pombe na kulewa mpaka kubakwa kilikuwa ni cha aibu mno ambacho alishindwa kumshirikisha mtu mwingine! Mama yake alipompigia simu alijikaza na kuongea kama mtu asiyekuwa na matatizo na hata Kevin pia hakugundua chochote, Catarina akaamua kufa na siri moyoni, ingawa hofu juu ya kuwa ameambukizwa ama kutokuambikizwa virusi vya ukimwi ilibaki ikimsumbua na hakuwa tayari kwenda kupima.
Siku tatu mfululizo hakula, alibaki amejifungia chumbani kwake na kulia, siku ya nne ndipo Mkurugenzi wa Kampuni ya Mitindo ya Fonex Modeling, Teddy Khumalo alilazimika kufika nyumbani kwake kumwona, tena akiongozana na Craig, alitaka kufahamu sababu ya Catarina kutofika ofisini kwa siku tatu mfululizo.
“I am sick!”(Naumwa!)
“What are suffering from?”(Unaumwa nini?)
“Lower abdominal pain!”(Tumbo la chini!)
“Can I take you to hospital?”(Naweza kukupeleka hospitali!)
“No! I will be okay!”(Hapana! Nitakuwa sawa!)
“Are you bleeding?”(Uko kwenye hedhi?)
“Yeah!”(ndiyo!)
“Sorry ! Get well soon because we have a trip tu Paris for Paris Fashion week, you will be showing Mario Pizaro’s designs, you know him?”(Pole! Pona upesi sababu tutakuwa na safari ya kwenda Ufaransa kwenye wiki ya mitindo ya Paris, utakuwa ukionyesha mavazi ya Mario Pizaro, unamfahamu?)
“Yes!”(ndiyo!)
“Ok! Bye!”(Sawa! Kwaheri!)
Craig hakuongea maneno mengi zaidi ya salamu, uso wake ulionekana kujawa na aibu, hata hivyo, uamuzi wa Catarina kudanganya ulimpa ahueni kuwa alikuwa ameamua kuficha ukweli wa kilichokuwa kimetokea. Walipoondoka, Catarina alianza kuifikiria Ufaransa na Mario Pizaro, ambaye kwa miaka mingi alikuwa amesikia habari zake na sasa alikuwa anakwenda kukutana naye ana kwa ana, maumivu yote ya moyo yakapungua, alichokipanga moyoni mwake kwa sababu alikuwa akihitajiwa na makampuni mengi ya mitindo duniani, ni kutafuta wakala mwingine akiwa nchini Ufaransa.
Wiki mbili baadaye walipanda ndege ya shirika la ndege la Ufaransa kuelekea Paris, bado Catarina akiwa amejawa na huzuni, fikra zake zikiwa juu ya Kevin na hali yake ya afya, bado alikuwa haongei vizuri na Craig na alidhamiria kutafuta wakala katika nchi nyingine duniani ili aondoke mikononi mwake, hakutaka kabisa kumwona tena.
Je, nini kitaendelea? Fuatilia siku ya Jumatano katika Gazeti la Championi Jumatano.
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO, BOFYA HAPA ===>https://www.facebook.com/shigongotz/