Beki tegemeo wa timu ya Yanga, Kelvin Yondani.
KAMATI ya Usajili ya Yanga, imestopisha mazungumzo yake na beki tegemeo wa timu hiyo, Kelvin Yondani kuhusu kumuongezea mkataba mpya utakaomwezesha kubaki klabuni.
Sababu kubwa ya kusitisha mazungumzo hayo imeelezwa kuwa ni kuweka umakini zaidi katika kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara ambao pia unawaniwa na Azam FC na Simba.
Mabosi wa Yanga wameona haitakuwa busara kumchanganya Yondani aliyetua klabuni hapo msimu wa 2010/11 kutoka Simba, kwa mazungumzo ya mkataba badala yake watazu ngumza naye baadaye.
Yondani amebakisha miezi sita katika mkataba wake na kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka Kimataifa (Fifa), beki huyo mkongwe anaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine inayomhitaji.
Mmoja wa viongozi wa Yanga aliliambia Championi Jumamosi kuwa, walianza mazungu
mzo kwa ajili ya kumuongezea mkataba Yondani lakini wamesimamisha ili kupisha mechi mbili za ligi kuu dhidi ya Simba na Azam.
Chanzo hicho kilisema, kikubwa wanataka beki huyo akili zake aelekeze kwenye mechi za ligi kuu wakati timu hiyo ikipambana kutetea ubingwa wake wa ligi kuu.
“Yondani tulishafanya naye mazungumzo ya awali kwa ajili ya kumuongezea mkataba wa kubaki Yanga, lakini sisi kama uongozi na yeye mwenyewe tumefikia mahali pazuri na ameomba tumalizie ligi kwanza.
“Tumehofia tunaweza kumtoa mchezoni, kwa sababu tutakapoanza mazungumzo hayo, basi lazima tuzungumzie kiasi cha fedha atakachokihitaji na mahitaji mengine, hivyo tungemvuruga.
“Uzuri wake yeye mwenyewe Yondani ametuhakikishia kuwa hatakwenda popote na badala yake atabaki kuichezea Yanga kutokana na mapenzi yake na klabu,” alisema kiongozi huyo.
Alipoulizwa Yondani kuhusu mkataba wake, alisema: “Ni kweli mkataba wangu unaelekea ukingoni, lakini siwezi kuuzungumzia hivi sasa, akili yangu nimeelekeza kwenye ligi.”
Your Comment-Simba tukomae bingwa wetu mwaka huu