×

Amanda amkubali Mr. English

Na mwandishi wetu, Risasi Jumamosi
STAA wa Bongo Muvi, Tamrina Posh ‘Amanda’ amefunguka kuwa anakubali kazi inayofanywa na mtaalam wa Kiingereza, Qrian James ‘Mr. English’ kuwanoa mastaa.

Akimzungumzia Mr. English anayefundisha Kiingereza cha kuzungumza kwa muda wa siku 10 tu, Amanda alisema ni vizuri mastaa na hata watu wa kawaida kumuona mtaalam huyo kwani Kiingereza kina msaada mkubwa kimataifa.

“Nimekwenda pale Sinza Lion, nimeona anavyofundisha. Hata mimi nimeguswa kujifunza, niwashauri mastaa wengine wajifunze kwa njia kama hii ya haraka ili kuweza kuliteka soko la kimataifa,” alisema Amanda.

Leave a Comment