×

Mr TZ Apiga Picha za Utupu

STORI: Mwandishi
Wetu, Risasi
DAR ES SALAAM: Picha za utupu zinazomhusu mwanamitindo maarufu Bongo, aliyewahi kunyakua mataji kadhaa ya mitindo, likiwemo la Mr Tanzania, Next Handsome Man 2013/2014, Lota Mollel zimevuja mtandaoni na kusababisha gumzo kubwa kwa walioziona, Risasi Mchanganyiko limezinasa.

Katika picha hizo, mwanamitindo huyo anaonekana akiwa katika mapozi tofautitofauti, akiwa hajajisitiri kwa nguo hata moja, jambo ambalo ni kinyume na maadili ya Kitanzania, ukizingatia yeye ni kioo cha jamii.
Baada ya Risasi Mchanganyiko kuzinasa picha hizo, iliamua kujiridhisha kama kweli aliyekuwa anaonekana ni Lota ambapo ilibidi paparazi wetu aingie mtaani kumsaka mwanamitindo huyo, baada ya simu yake kutokuwa hewani kwa muda mrefu.

Baada ya kuoneshwa picha hizo, Lota alikiri kuzifahamu na kueleza kwamba kweli ni zake lakini alizipiga kwa ajili ya shughuli zake za sanaa.
“Kwanza wewe umezipata wapi? Hakuna mtu aliyekuwa anazijua hizi picha, nilikuwa nimezihifadhi kwenye simu yangu iliyopotea kwa ajili ya kazi zangu za uanamitindo,” alisema Mollel akionesha kufadhaika.
Alipoulizwa ni mitindo gani inayoruhusu mtu kupiga picha za utupu kabisa na ilikuwaje mpaka picha hizo zikavuja, Lota aliishia kusema kwamba simu yake ambayo ndiyo iliyokuwa na hizo picha, ilipotea klatika mazingira ya kutatanisha na kwamba halikuwa kusudi lake kuzivujisha mtandaoni.

Leave a Comment