STAA wa Muziki wa R&B, Benard Paul ‘Ben Pol’.
STAA wa Muziki wa R&B, Benard Paul ‘Ben Pol’ amefu-ngukia ngoma yake na Juma Musa ‘Jux’ ya Nakuchana kuwa haikuwa rasmi katika kuiachia redioni kwani walikuwa wakifanya kama utani.
kama utani.
Akichonga na Showbiz Xtra Ben Pol alisema, waliamua kurekodi ngoma hiyo kwa lengo la kujifurahisha huku wakiirusha kwenye mitandao ya kijamii, hali iliyosababisha kusambaa kwa kasi na kukubalika zaidi kwa mashabiki.
“Tulikubaliana kuandika mistari na Jux na kuamua kuimba huku tukirusha vipande kwenye mitandao kama majibizano f’lani, baada ya muda mfupi wimbo huo ukasambaa zaidi huku watu wakipendekeza kurushwa wote, ndipo tukaamua kumalizia,” alisema Ben Pol.