STAA wa Bongo Fleva, Abednego Damian ‘Belle9’.
Imelda Mtema
STAA wa Bongo Fleva, Abednego Damian ‘Belle9’ kwa mara ya kwanza amefunguka kuwa anajuta kitendo cha kutojichanganya viwanja kipindi cha nyuma kwani alikuwa akikosa mengi ya kujifunza hususan kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva.
Akipiga stori na Showbiz Xtra, Belle9 anayebamba na Ngoma ya Burger Movie Selfie alisema hayo hivi karibuni katika shoo yake ya Love Portion iliyofanyika pande za Sky Night Life, Masaki kuwa ndani ya kipindi kifupi alichorudi kwenye gemu baada ya kuwa kimya kwa kipindi kirefu kumemfanya kutojua mambo mengi.
“Nilikuwa si mtu wa kujichanganya na wasanii wenzangu kwenye sehemu kama hizi, lakini leo hii kidogo tu nimeona tofauti kubwa na nimejifunza mengi,” alisema Belle9.