Staa wa filamu Bongo, Chuchu Hancy.
Na Imelda Mtema
Staa wa filamu Bongo, Chuchu Hancy amefunguka kuwa usaliti aliokutana nao katika uhusiano wa kimapenzi umemfanya akomae zaidi hivyo kutotetereka.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Chuchu alisema kuwa maisha yake ya kimapenzi yana simulizi nzito sana huku sehemu kubwa ikiwa ni kuumizwa na wanaume ndiyo maana sasa hivi anao uwezo wa kukabiliana na changamoto yoyote kwenye maisha ya kimapenzi.
“Yaani acha tu, maisha yangu ya kimapenzi yana historia kubwa huku usaliti ukichukua nafasi kubwa ndiyo maana nimeamua kutunga thamthiliya ya usaliti ambayo inaweza kuelezea kila kitu kuhusu mimi, imeshaanza kurushwa hewani kupitia EATV,” alisema Chuchu.