Richard Bukos
INADAIWA kuwa zaidi ya shilingi milioni saba zimesa-babisha kutiwa mbaroni msanii wa Muziki wa Dansi Bongo, Alain Mulumba Kashama mwishoni mwa wiki iliyopita na Idara ya Uhamiaji kwa madai ya kulimbikiza malipo ya kibali cha kuishi nchini.
Akizungumza na Showbiz Xtra, swahiba wa mwanamuziki huyo, Totoo Ze Bingwa alisema kuwa, Mulumba alidakwa akiwa mazoezini na bendi yake ya BMM Ngwasuma na kwenda kuswekwa Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati ‘Centro’, Posta jijini Dar.
“Wajua, Mulumba anadaiwa kulimbikiza malipo ya kibali chake cha kuishi hapa nchini ambapo deni hilo limefikia zaidi ya milioni saba, lakini taratibu za kumtoa zinaendelea kufanyika,” alisema Ze Bingwa.
Jitihada za kumpata Mulumba zilishindikana na hata alivyotafutwa kwa njia ya simu hakupatikana hewani.