×

Global FC, KKKT Pwani watoka suluhu mechi ya kirafiki

 

 

5.Kikosi cha Timu ya KKKT Usharika wa Pwani kinavyoonekana.

3.Global FC ikipiga picha kabla mchezo kuanza.Kikosi cha Timu ya Global FC.

6.Mchezo ukiwa umeanza baina ya timu hizo mbili.7.Mtanange ukiendelea.
8.Timu ya KKT Usharika wa Pwani ikiwa mapumziko wakati wa kipindi cha Pili.Timu ya KKKT Usharika wa Pwani ikiwa kwenye mapumziko kabla ya kipindi cha Pili.

9.Viongozi wa Timu ya Global FC wakitoa ushauri kwa wachezaji wao.Viongozi wa Timu ya Global FC, Amran Kaima (Kushoto) na Elvan Stambuli wakitoa maelekezo kabla ya kuanza kipindi cha pili.10.

TIMU ya Global FC na KKKT Usharika wa Pwani, jana Ijumaa zilitoka suluhu ya bila kufungana katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Bora, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kuvutia, Global iliutumia kama sehemu yao ya maandalizi ya michuano ya NSSF inayotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao.

Baada ya kumalizika kwa mchezo huo, nahodha wa KKKT, Godwin Sinda amesema: “Tunashukuru kwa mchezo huu kumalizika salama, nadhani sababu kubwa iliyotufanya tusiibuke na ushindi ni kutokana na kuchelewa kufika uwanjani kwani ilitupelekea kuingia uwanjani bila ya kupasha misuli.

“Yote kwa yote bado tupo katika kuijenga timu yetu kwani tangu tuanze kuijenga hii ni mechi ya pili, ya kwanza tulishinda 5-3 dhidi ya Vijana Kinondoni, lakini kutokana na Global kuonesha uungwana bila shaka tutawaomba tena mechi nyingine ya kirafiki.”

Naye nahodha wa Global, Philip Nkini, alisema: “Tunaendelea vizuri katika kujiandaa na mashindano ya NSSF, tunawaomba wapenda michezo wote wajitokeze kutupa sapoti katika hili.”

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave a Comment