×

Niyonzima ampa Mkude neno la mwisho

NIYONZIMANEW4Haruna Niyonzima.

Hans Mloli, Dar es Salaam
MOJA kati ya vitu vitakavyotazamwa sana leo ni vita ya viungo wa Simba na Yanga katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika kiungo, Simba itakuwa na Jonas Mkude na Mwinyi Kazimoto wakati Yanga inao Thabani Kamusoko na Haruna Niyonzima, hapo kazi ipo na watachuana kwelikweli.
Lakini kiungo wa Yanga, Niyonzima ameliambia Championi Jumamosi kuwa, anafahamu na kuheshimu uwezo wa wapinzani wake lakini atahakikisha anafanya vizuri kuwapiku ili washinde.
Niyonzima hakutaka kufafanua zaidi kuhusiana na uwezo wa wachezaji hao zaidi ya kusisitiza kuwa watakutana uwanjani leo katika mchezo huo wa ligi kuu.
“Mkude ni mchezaji wa kawaida tu, nafikiri tusubiri tutaona uwanjani lakini kwa ujumla, mechi ni ngumu ila sisi kama wachezaji tunajiandaa vizuri kupata ushindi.
“Kombinesheni yangu na Kamusoko naiona ni nzuri tu kwa sababu tunajuana muda mrefu, kwa hiyo inakuwa rahisi kuelewana zaidi tukiwa uwanjani,” alisema Niyonzima, raia wa Rwanda.
Siku chache zilizopita, Mkude alinukuliwa na gazeti hili akiitahadharisha safu ya ulinzi ya Yanga kwa kusema: “Tumebadilika, sasa tupo vizuri na kila mchezaji ana hamu na ushindi.”

Leave a Comment