ILIPOISHIA GAZETI LA RISASI JUMAMOSI:
Nilikwenda sebuleni na kuchuchumaa ili kuonesha adabu mbele ya wenye nyumba ambao ni mabosi wangu…
“Hivi wewe huna simu?” aliniuliza baba Rehema…
“Sina baba.”
“Mama Rehema, huyu anunuliwe simu haraka sana. Hata ya tochi. Sasa kama hana simu ina maana tukiwa hatupo na kuna dharura anatupataje?”
Palepale nilimwona mama anasimama na kunifuata huku akiwa amenitolea macho.
JIACHIE MWENYEWE SASA…
Nilitaka kusimama ili nikimbie, lakini sijui moyo wa ujasiri niliutolea wapi, nikakaa nikimwangalia tu.
“Hivi wewe ni nani kwenye ndoa yangu mpaka upewe kipaumbele cha hivyo,” alisema kwa ukali mama Rehema…
“Mama Rehema mguse uone kitakachokupata,” baba Rehema aliingilia kati kwa sauti ya kiume iliyotoka kwa mamlaka ya hali ya juu.
Nilimwona mama Rehema akienda chumbani na kuniacha sebuleni mimi na mume wake. Aliniangalia baba Rehema akaachia tabasamu…
“Huyu atapita kwenye rula mpaka atakoma,” alisema baba Rehema nikiwa sijui maana ya kupita kwenye rula…
“Kupita kwenye rula maana yake nini?” nilimuuliza…
“Yaani atanyooka tu!”
Baba alisimama, akanifuata, akanibusu na kuniambia…
“Nenda kalale sasa baby.”
“Asante sana,” nilimshukuru nikisimama na kwenda chumbani kwangu. Nilimwacha baba Rehema sebuleni na wala sikufuatilia aliondoka muda gani bali wakati nakuja kushtuka, kitasa cha mlango wa chumbani kwangu kilikuwa kikichezeshwa kiasi kwamba nikahisi kuna mtu kwa nje.
H
ali ilivyoendelea nilitoka kitandani kwani nilijua kwa vyovyote vile atakuwa baba Rehema kwa hiyo isingekuwa rahisi mimi kuuliza nani.
Nilifungua mlango huku nikitetemeka na moyoni nikisema…
“Huyu sasa anataka balaa. Je, mke wake mama Rehema akiamka na kumkosa kitandani akaamua kuja huku akamkuta itakuaje? Au kamfungia kwa nje?”
Nilifungua mlango na hamadi nilikutana na uso wa mama Rehema…
“Tuingie ndani kwako Jamila,” alisema kwa sauti ya chini huku akinisukuma.
Nilirudi kitandani, nikakaa…
“Jamila,” alianza kuniita…
“Abee…”
“Unaniheshimu?” aliniuliza.
“Ndiyo mama.”
“Kama ni ndiyo niambie ukweli una uhusiano wa kimapenzi na mume wangu baba Rehema?”
“Mimi sina mama…”
“Mbona yeye kakubali?”
Nilishtuka sana kusikia mama Rehema akisema baba amekubali kwamba mimi na yeye tuna uhusiano wa kimapenzi, nikataka kumwambia kama baba amekubali basi ni kweli, lakini roho ikasita…
“Kama amekubali yeye mimi sijakubali bado. Na sijawahi hata kufikiria kama kuna kitu hicho, mimi namheshimu sana baba Rehema. Namchukulia kama baba yangu mzazi, sasa kwa nini nifanye hivyo na kwa nini yeye anisingizie vitu vya uongo? Mimi nikiamka asubuhi lazima nimuulize.”
Nilimwona mama akianza kunywea kuhusu msimamo wangu…
“Sina maana umuulize. Kwanza ujasiri wa kumuuliza mtu mzima kama huyu mume wangu utaupatia wapi wewe?” mama alitaka kunigeuzia kibao cha nguvu.
“Mama, yeye si ndiyo amenisingizia uongo mimi? Kwa nini nisimuulize?” nilimchachamalia nikianza kuamini kwamba, alikuwa akisema uongo kuhusu baba Rehema.
Kwa jinsi alivyo isingekuwa jambo rahisi waongee chumbani halafu baba Rehema aseme mimi na yeye ni wapenzi. Kwanza nyumba yote ingekuwa inawaka moto.
Mama Rehema alisimama maana naye alikaa huku akisema…
“Sitaki umuulize jambo lolote mume wangu. Nitakukata sikio.”
***
S
aa moja na nusu asubuhi nikiwa nafagia uani, baba Rehema alitokea, akanishika wowowo. Maana mimi naye, licha ya kuwa msichana wa kazi za ndani lakini nilikuwa wa kuangaliwa mara mbili.
Kwanza nilibahatika kwenda hewani kumpita mama Rehema. Pili, sikuwa mnene kama mama Rehema. Maana nilikuwa sipendi kulakula. Tatu, nilijaliwa wowowo la haja! Nne, niliumbwa kwa kukatika katikati. Nikiwa sijavaa nguo ungeweza kusema unaangalia umbo namba nane! Acha kabisa!
“Mbona umeshtuka sana?” aliniuliza baba Rehema…
“Umenishtua sana, nikakumbuka jana pale kitandani,” nilimwambia nikichekacheka.
Moyoni nilidhamiria kabisa kuisambaratisha ndoa ya mama Rehema sasa kutokana na mambo anayonifanyia. He! Mwanamke gani hanipi uhuru hata kidogo. Mchana kutwa, usiku kucha yuko na mimi kutafuta mabaya yangu tu!
“
Unapenda na leo tena?” aliniuliza…
“Kwani huendi kazini?” na mimi nilimuuliza kabla sijamkubalia…
“Naweza kuwahi kurudi.”
“Poa tu. Mama Rehema atakuwa wapi?”
“Si anapendaga kutoka?”
“Haya sawa!”
Baba Rehema aliondoka. Baadaye nikagundua alishakwenda kazini. Nikaumia sana kwamba alikwenda bila kuniaga.
***
Ilikuwa saa tano na nusu asubuhi, baba Rehema alirudi akiwa na boksi lenye simu mpya ndani yake. Mama Rehema hakuwepo muda huo…
“Jamila, nimekuletea simu,” baba Rehema aliniambia.
Kwa furaha nilisimama, maana alinikuta nimekaa sebuleni, nikaenda kumkumbatia kwa nguvu zangu zote mpaka tukaangukia kwenye kochi kubwa puuu..!
Kwa kweli chumbani kulikuwa mbali sana, wote tulijikuta palepale sebuleni tukizama kwenye denda sasa huku nikimshukuru sana baba Rehema kwa simu japokuwa nilikuwa sijaiona kwa macho zaidi ya boksi…
“Hivi kwa nini huyu Jamila hajafunga geti?” sauti ya mama ilisema huku ikishika mlango mkubwa wa kuingia sebuleni tulipo…
Je, unajua nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi Jumamosi.
Mbona sehemu ya 6 haipo?