×

Tamasha la Changia Damu Salama Lafikia Kilele Chake

damu (1)

Zoezi la kujitolea kuchangia damu likiendelea.damu (2)Watu wakishuhudia tamasha hilo na kusikiliza maelekezo mbalimbali.damu (3)

damu (4)Wasanii wakitumbuiza.damu (5)

Mmoja wa watu waliojitolea kutoa damu akichukuliwa vipimo vya awali.

HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini, leo wamefikia tamati ya tamasha la kuchangia damu lililofanyika Karume jijini Dar.

Tamasha hilo lililokuwa na kauli mbiu ya ‘Changia Damu Okoa Maisha’ limelenga kuimarisha benki ya damu ambayo ina upungufu mkubwa wa damu sambamba na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa uchangiaji wa damu.

Akizungumza na mwandishi wetu, Msaidizi wa Uhamasishaji wa Kuchangia Damu, Sebastian Magulu wa Kitengo cha Huduma ya Dharula kutoka Hospitali ya Muhimbili alisema kuwa, watu wengi hawana mazoea ya kuchangia damu suala ambalo linarudisha nyuma jitihada za madaktari kuokoa maisha ya wagonjwa wengi wanaokutwa na tatizo la upungufu wa damu.

Akizungumzia faida za kuchangia damu, Sebastian alisema kuwa kwa kufanya hivyo kunamfanya mtu aokoe maisha ya mtu mwingine na kuongeza kuwa mtu yeyote atakayejitolea damu atapata kitambulisho maalumu kitakachomuwezesha apatiwe huduma ya kuongezewa damu popote atakapohitaji kupatiwa huduma hiyo.

Picha/ Chande Abdallah

Leave a Comment