×

Nilivyoivunja Ndoa Yangu na Shetani-17

ILIPOISHIA:

 

Mara alitokea mwanaume mmoja aliyekuwa amevalia kaptula iliyovuka magoti, juu alikuwa kifua wazi na kuonesha michoro ya tatuu mkononi alikuwa na glasi iliyokuwa na pombe ndani.

 

SASA ENDELEA…

 

“Leo naona tuna mugeni mupya?” yule bwana aliuliza kwa lafudhi ya Kilingara.

“Ndiyo Papaa.”

“Ni mutu ya wapi?”

“Ya Tizedi.

“Ooh! Simama mrembo,” alinieleza nisimame anione nami nilifanya vile.

“Tembea kidogo.”

Nilifanya kama alivyotaka kwa madaha nilijua kauvaa moto wa gesi. Nilijiamini kwenye kazi ile si kwa mitego tu hata kumkata kiu mwanaume. Kila mwanaume aliyeuonja mwili wangu hakuonja mara moja nilikuwa na asili ya asali. Baada ya kutembea na kusimama nilijigeuza kwa madaha huku wote wakipiga kelele.

“Waaaooo!”

“Uko murembo, Josee, mupeleke chumbani kwangu,” Papaa alitoa amri.

Yule kijana aliyekuwa akinihoji kwanza alinishika mkono na kunipeleka chumbani kwa bosi wao. Tukiwa tunaelekea huko yule kijana alinieleza kitu:

“Mrembo, ningejua nisingekuleta huku.”

“Kwa nini?”

“Nilitaka niwe na wewe lakini basi kachukua mzigo wangu.”

“Tatizo nini?”

“Bosi amewahi.”

“Basi wewe siku nyingine.”

“Sijawahi kukutana na mwanamke mzuri kama wewe.”

“Mmh! Mi mbona wa kawaida.”

“Hapana ndo maana bosi kakuchukua huwa haingilii wanawake tunaowaleta.”

“Basi kesho zamu yako,” nilijitafutia mteja wa kesho yake kabisa.

“Nipe namba ya simu.”

“Simu sina.” Aliingiza mkono mfukoni na kunikabidhi pesa ambazo sikujua zipo kiasi gani na kunieleza ninunue simu ili tuwasiliane.

“Poa.”

“Kesho nisubiri usiondoke na mtu sawa mrembo?”

“Sawa.”

“Acha nitoke kabla bosi hajashtuka.”

“Poa.”

Aliniacha chumbani na yeye kutoka nje, kwa vile chumbani kulikuwa na kochi niliona sehemu ile inafaa japokuwa shughuli iliyonipeleka pale mafikio yake ni kitandani. Baada ya muda bosi aliingia chumbani na kuja moja kwa moja nilipokuwa nimekaa na kunibusu shavuni.

“Karibu murembo.”

“Asante.”

“Leo macho yangu yamemuona mwanamke muzuri wa sura na umbile.”

“Asante sana.”

Kabla ya kufanya yetu nilizumgumza mengi na Papaa aliyesema kuwa nijiite mwanamke mwenye bahati. Nilimuuliza kwa nini nijiite mwanamke mwenye bahati.

“Huwa sichukui mwanamke aliyeletwa na vijana wangu, lakini ajabu wewe umeniteka ghafla.”

“Ooh!”

“Sasa mrembo kuna kitu cha ziada nimekiona kwako, kuna biashara tutaifanya ikienda vizuri nitakupa asilimia kumi ya kile utakachokiingiza.”

“Mmh! Sawa ni biashara gani au kuuza madawa ya kulevya?”

“Walaa ni uwezo wako wa kupokea maelekezo na kuyafanyia kazi, ushawahi kuigiza?”

“Sijawi lakini uigizaji nauweza kuliko hata hao waigizaji, kwani una filamu yako?”

“Walaa, ila utajua tu nina imani kazi ya kuuza mwili utaiacha, mwanamke muzuri kama wewe unatakiwa uwe chini ya mwanaume ule maisha.”

“Sijapata.”

“Muda umekimbia sana tule vyetu, nina imani kesho tutazungumza mengi.”

Kwa vile kulikuwa kuna kazi maalum imenipeleka pale tulifanya yetu bila kukubaliana bei. Sikuwa na wasiwasi niliamini shughuli nitakayompa itamrusha akili na kunipa pesa nyingi. Mpaka tunalala palichimbika bila jembe na kutuacha wote hoi huku nikijifikiria siku inayofuata kama nitaweza kusimama usiku kutokana na uchovu.

Ilikuwa tofauti na taratibu za kwenda kulala nje na mteja, ilitakiwa saa kumi akuachie ili alfajiri ikukute nyumbani kutokana na mavazi yetu. Nilishtuka usingizini  na kujikuta peke yangu kitandani. Nilijiuliza mwenyeji wangu yupo wapi.

Baada ya kutulia kitandani kwa zaidi ya robo saa bila kumuona niliamka na kwenda kuoga kisha nilivaa nguo zangu na kutoka chumbani hadi sebuleni.  Nilimkuta mwanamke aliyekuwa amevalia kitawa akifanya usafi kwa kupanga vitu vizuri vilivyokuwa sebuleni.

Kilichonishtua kifuani kwake kulikuwa na msalaba mkubwa kuonesha ni mcha Mungu, nilijiuliza pale ni wapi mbona kulikuwa na dalili zote za kuonesha eneo lile ni la wacha Mungu. Nilibakia nimesimama nikiwa nimepigwa butwaa, yule mdada baada ya kuniona alinisalimia kwa unyenyekevu.

“Habari dada?”

“Nzuri.”

“Sa…sa…maha…”

“Bila samahani dada angu, naomba unifuate.”

“Sawa,” nilijibu na kumfuata.

Tuliingia katika chumba kimoja kilichoonekana ni cha kulala, baada ya kuingia yule dada alinieleza:

“Samahani dada naomba ubadili hizo nguo.”

“Kwa nini?”

“Utajua baadaye.”

“Kwani mwenyeji wangu sijui anaitwa Papaa yupo wapi?”

“Ametoka ghafla.”

“Sasa ametokaje bila kuniachia pesa yangu,” nilikuwa mkali kidogo.

“Dada pesa si tatizo, sema ametoka ghafla ila kaacha maagizo.”

“Maagizo gani?”

“Kuna dereva atakufuata na kukupeleka kwako.”

Je, nini kitaendelea? Usikose siku ya Jumatano.

Leave a Comment