Staa wa Hip Hop Marekani, Tyga.
LOS ANGELES, Marekani
BAADA ya maswali mengi kwa staa wa Hip Hop Marekani, Tyga kuhusiana na kujihusisha kimapenzi na modo Kylie Jenner, 19, wakati akiwa na umri mdogo, rapa huyo ametolea ufafanuzi ishu hiyo.
Modo Kylie Jenner.
Tyga alianza uhusiano na Kylie mwaka jana wakati mrembo huyo akiwa na miaka 18 jambo ambalo lilikuwa likipingwa kwa madai kuwa modo huyo alikuwa mdogo kiumri hivyo angeshindwa kufanya maamuzi mbele ya staa huyo wa Hip Hop.
Akifanya mahojiano na Kituo cha Redio cha 106 KMEL cha Marekani, Tyga alisema hakuzungumza suala hilo kwa kuwa umri haukua kitu rasmi sana alivyoanza uhusiano naye.
“Sikuweza kuongelea hili suala mapema sababu kila mtu alitaka kuponda na kuhukumu. Sijui kwa nini wakati mimi nilikuwa namuona ni mtu mzuri.”