×

Denti azaliwa na gonjwa hatari kutoka mikoani

Mtoto gonjwa mwanza (1) Hassan Mharami na mama yake mzazi, Mariam Bujimu.

Na Idd Mumba, AMANI

MWANZA: Kweli Mungu ndiye muweza wa kila jambo! Mwanafunzi wa darasa la saba kwenye Shule ya Msingi Chamwenda, Hassan Mharami anateseka kwa ugonjwa wa ajabu kufuatia kuzaliwa akiwa na magamba mwili mzima.

Hassan ambaye ni mkazi wa Uwanja wa Mbuzi-Kiloleli wilayani Ilemela mkoani hapa alizaliwa na ugonjwa ambao unamfanya aonekane kama anaota miti mwilini. Mama mzazi wa Hassan, Mariam Bujimu anasimulia kwa undani namna mwanaye alivyozaliwa na ugonjwa huo, maendeleo yake na anavyoteseka.

Mtoto gonjwa mwanza (2)Hassan Mharami.

“Hali hii ya mwanangu ilianza kujitokeza tangu alipozaliwa tu kwani alionekana kuwa na magamba malaini mwilini.

“Awali, kama mzazi nilishindwa kubaini mara moja nini kilimpata mtoto wangu, lakini kadiri siku zilivyozidi kusonga mbele ilibidi nimpeleke Hospitali ya Rufaa ya Bugando ili akapatiwe matibabu.

“Lakini sikufanikiwa kwani madaktari wa pale walisema tutafute hospitali nyingine kwa kuwa, wao hawakugundua tatizo la ugonjwa huo.

“Niliendelea kuhangaika katika hospitali nyingine za hapa Mwanza ili mwanangu apone lakini bila mafanikio. Ikabidi nimpeleke hospitali moja iliyopo Moshi, Kilimanjaro,” alisema mama Hassan.

Mama huyo aliendelea kusema kuwa, madaktari wa hospitali hiyo walimpa dawa ambayo ilimsaidia kidogo mtoto wake lakini baada ya muda ugonjwa ulimrudia hali iliyowalazimu kurudi tena Moshi kupata dawa hizo.

“Lakini dawa mara ya pili hazikumsaidia tukalazimika kwenda kupima ugonjwa wa ngozi, akapewa mafuta ya kupaka. Tatizo lilipungua kidogo tu kisha likarejea kama awali. Kwa kweli nimeteseka sana na mwanangu na bado tatizo lake halijapatiwa ufumbuzi.

“Ukiangalia hali ya maisha ni ngumu na gharama za kumpeleka nje ya nchi kwa ajili ya kutibiwa hatuna uwezo wa kumudu hivyo tunawaomba Watanzania watakaokuwa na uwezo hata wa kututafutia dawa zitakazowezesha kupona kwa mwanangu atusaidie na Mungu atamlipa.”

Naye Hassan alisema kuwa, ugonjwa huo umemfanya ashindwe kujiamini katika maisha yake kwani wakati wa usiku mwili unawasha na anashindwa kulala huku baadhi ya watu wakimtenga na kumnyanyasa kutokana na hali hiyo.

“Lakini namshukuru Mungu, kuna baadhi ya watu, walimu na wanafunzi wenzagu wananipa ushirikiano mzuri mpaka najisikia furaha ya maisha,” alisema Hassan.

“Lakini ukweli ni kwamba, ugonjwa wangu hauambukizi kwani ungekuwa wa kuambukiza familia yangu na wanafunzi wenzangu ningewaambukiza.

Kwa yeyote atakayeguswa kwa kujua Mungu ndiye muweza awasiliane na mama yake kwa namba; 0752 298 732.

3 Comments

  1. Pole sana Hassan na mama pia. Ni YESU peke yake anayeweza kumponya Hassan.
    Namshauri mama Hassan na Hassan waende kanisa linalohubiri wokovu wa YESU KRISTO na wanaoamini katika uponyaji kwa Damu ya YESU na Hassan ataponywa kabisa. DAKITARI WA KWELI NI YESU TU!

  2. Pole sana Hassan,mateso unayoyapata ni makubwa sana..ww pekee ndiyo unayeyajua mateso hayo.Ushauri alioutoa dada Upendo hapo ndio suluhisho pekee.unaweza kwenda hata huko India na wasiweze kukuponya pia,naamini utapona ukiamini kuwa damu ya Yesu ndio pekee inayoponya magonjwa yote,hata yale yaliyowashinda madaktari bingwa wa dunia hii..mfano mzuri muigizaji wa video za kibongo Saladini ..baada ya kuhangaika sana ameponea kanisani baada ya maombi..
    Tafadhali usipuuzie ushauri huu…nenda mwenyewe kwenye kanisa lolote linalotangaza wokovu wa Yesu Kristo..

Leave a Comment