Mambo vepe masela na wana wote wa kitaa cha bee. Si ni mzuka arifu? Kwani nini mbaya? Basi kipande hii haina kwere machizi wangu. Kama vepe njooni saidi hii tupige mastori yetu dizaini tujue tunachomokaje sasa mazee?
Wanangu si mbishe za kusaka mabovu zimeshika kasi? Huo ndo mpango mzima na hakuna kusanda mazee. Cha msingi tukaze tu chama langu la kitaa kozi wani dei yesi!
Kwenye mastori yetu tudei hapa ubaoni kwa fasi ya jamvini, kachala wangu mmoko ana bonge la ishu inayompa stresi za kufa mtu. Selaa anakuteli kuwa alikuwa na mkiksi wake mkare kinoma ambaye alikuwa amemingo naye kwa miaka kibwena wakitumbua tu hepi laifu.
Unaambiwa mshkaji alikuwa anamlavu shori wake ileile kiasi kwamba hakuwahi kusanuka kwamba ipo dei manzi angezingua na kuanza kesebenza na chalii mwingine kwa mpango wa kando.
Sasa bana katika hizi mbishe za kusaka laifu, mwana alipata zali la kwenda kupiga klasi mambele. Shori akampa maviapo kibwena ili jamaa yangu awe mwaminifu huko mamtoni dheni na mtoto mkare naye akampromisi mshkaji kutomaindisha mambo f’lani ya mameni.
Wakati mzazi jembe anatimua Bongo tambarare ishu zilikuwa poa kinoma na hata alipotimba mamtoni waliendelea kupiga mastori kwa foni na kurushiana mapicha matamumatamu. Si unajua zile za kubipu na kula tu wepesi?
Miezi bee baadaye mwanangu alirejea malikizo nene na nene so misele ya kwenda auti na shori wake ndo ikawa mpango mzima.
Siku moko wakati wamechili kupoteza mastresi, msela alisapraizi kumuona mkiksi wake anapokea simu za kumwaga na kuchati kwa sana aisee arifu.
Basi bana, kachala wangu akaona isiwe kitu, akatumia maubabe kuchukua ile foni ya shori. Hapo ndo soo lilipoanzia. Unaambiwa jamaa alikutana na mameseji ya ajabu kinoma ya ule mchezo mbaya wa kiutu uzima ulivyokuwa ukichezwa karibia deile kozi jamaa mwingine alikuwa anamaindi kwamba shori hampi mavitu tangu msela amerejea kwa fasi ya kitaani.
Mazee unaambiwa chama langu aliishiwa nguvu kabisa akajikuta akiishia kupaniki na kupata mastresi ya kufa mtu. Unaambiwa shori naye anajua fiksi kinoma so akafanikiwa kumshika masikio mwanangu akaingia kwenye kumi na nane so akawa anasubiria dodo lidondoke chini ya mwarobaini.
Oya kama vepe mwana sanuka, acha kushikwa masikio kozi utadanja kwa mastresi. Kama ungekuwa ni wewe ungesanukaje sasa? Tafakari, chukua mastepu mwana.
Kama vepe sii yuu neksi wiki.