ILIPOISHIA WIKI ILYOPITA:
“Papaa! Paa! Papaaa! Pa!” ikafuatiwa na kilio kizito kisha chini ya mlango wa kuingia kwenye chumba hicho tukaanza kuona damu zinatoka.
SASA ENDELEA MWENYEWE:
Kusema kweli mimi nilishtuka sana, nikataka kupiga kelele za kuomba msaada lakini nilipokumbuka kwamba pale ni ujinini nikaacha kwani niliamini nisingeweza kupata msaada wowote na zaidi sana huenda ingechangia kifo changu.
“Mwingine.”
Ile sauti iliamuru tena, akaingia mwanamke mmoja ambaye alikuwa akitetemeka. Mlango ulipofungwa tu, tukasikia milio ya risasi. Mingi sana. Kama kuna watu walikuwa na bunduki, basi walizidi hata kumi kutokana na ile milio.
Ilipokoma kusikika, ikaja ile sauti ya kuamuru mtu mwingine aingie, mwanaume aliyekuwa mbele ambaye ilibidi aingie akarudi nyuma ya mtu aliyekuwa nyuma yake.
Sijui mimi niliupata wapi ujasiri nikajikuta nikisema mimi nakwenda. Lengo langu lilikuwa kujua kuna nini kule na je, tunayoyasikia ndiyo yanayofanyika kule ndani?
Niliwapangua watu kwenda mbele ili nikaingie mimi. Lakini kabla sijafika, nilisikia ile sauti ikisema ‘narudia tena, mwingine’.
Nilisukuma mlango, nikazama ndani lakini nilifikia kuanguka chini na kupoteza fahamu.
Ili kujua nini kilitokea, usikose kusoma wiki ijayo kwenye gazeti hilihili.
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO===>https://www.facebook.com/shigongotz/
KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA TUFOLLOW
INSTAGRAM===>https://www.instagram.com/globalpublishers/
TWITTER===>https://twitter.com/GlobalHabari
FACEBOOK===>https://www.facebook.com/GlobalPublishers
YOU TUBE===>https://www.youtube.com/user/uwazi1
Naitaji kitabu cha story cha shigongo naweza pata wapi
mhh fupi jamani