×

Bahati Nasibu Ya Shinda Nyumba Yatikisa Mbezi

WAKATI Bahati Nasibu ikiendelea kushika kasi, leo imeonekana kutikisa wakazi wa Mbezi ya Kimara na viunga vyake jijini Dar walionekana kuvutiwa nayo baada ya kujitokeza kwa wingi kuchangamkia magazeti ya Kampuni ya Global Publishers Ltd kwa kununua na kujaza kuponi kwa ajili ya kushiriki bahati nasibu hiyo.

Mara baada ya maofisa wa Global Publishers kufika maeneo ya Mbezi ya Kimara wasomaji wa Gazeti la Uwazi walijitokeza na kununua gazeti hilo kisha kujaza kuponi zinazopatikana kwenye ukurasa wa pili wa gazeti hilo huku pia wakijipatia zawadi za kofia zenye nembo ya Shinda Nyumba zilizokuwa zikitolewa.

Akizungumza na wakazi wa maeneo hayo Ofisa Masoko wa Global Publishers , Yohana Mkanda alisema: “Mnachotakiwa kufanya ni kununua magazeti ya Global na kujaza kuponi zinazopatikana ndani ya magazeti hayo ambayo ni Uwazi, Championi, Risasi Jumatano, Ijumaa Wikienda, Amani, Risasi Jumamosi na Ijumaa ambayo huuzwa kwa shilingi mia tano na msomaji anaweza kujishindia nyumba ya kisasa, kila anayejaza kuponi nyingi anajiongezea nafasi ya kujishindia nyumba hiyo iliyopo Salasala, Tegeta Dar na zawadi nyingine,” alisema Mkanda.

1Msomaji wa Gazeti la Uwazi aliyejitambulisha kwa jina moja la Philimon (kushoto) akijaza kuponi yake huku akipewa maelekezo kutoka kwa Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda.

2Mdau wa Gazeti la Uwazi, Alex Said (kulia) akisaidiwa kujaza kuponi yake na Ofisa masoko wa Global ili kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.

3Wasomaji wa Uwazi wa maeneo ya Mbezi Mwisho wakikata kuponi ili kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba .

4Ramadhani Mselemu (kushoto) akijaza kuponi yake ili kushiriki bahati nasibu hiyo.

5Kuponi zikiwekwa kwenye ndoo maalum ya bahati nasibu hiyo.

6Amani Hamis (katikati) akijaza kuponi yake huku ofisa masoko wa Global, Yohana Mkanda (kulia) akifuatilia kwa makini zoezi hilo la kujaza.

7Khalid Rajab (kushoto) akijaza kuponi yake ili kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.

8Wasomaji wa Gazeti la Uwazi walivyoonekana baada ya kumaliza kushiriki kujaza kuponi za bahati nasibu,ambapo walikuwa wakijisomea gazeti hilo.

Na Denis Mtima/Gpl

Leave a Comment