
Wauguzi, na madaktari wa Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana Butimba mkoani Mwanza wakiendelea na mgomo jana.


Wagonjwa wakiwa katika hali ya mshangao baada ya wauguzi, na madaktari kugoma.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga (katikati) akiongea na wagonjwa.

…Akiendelea kuongea.
…Wagonjwa kabla ya mkuu wa wilaya kufika.
Na Idd Mumba, Mwanza
Hali ya usalama katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana Butimba mkoani Mwanza kwa wauguzi, na madaktari sio nzuri na kusababisha wananchi kutopata huduma zaidi ya saa sita jana, jambo ambalo lilizua taharuki kubwa kwa wagonjwa na wananchi hospitalini hapo.
Mgojwa aliyejitambulisha kwa jina Janet John alisema wakifika katika hospitali hiyo ya saa moja asubuhi kwa ajili ya kupatiwa matibabu lakini hadi ilipofika saa tatu asubuhi hakukuwepo na daktari ama nesi aliyeingia katika vyumba vyao kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
‘’Sisi tumefika hapa hospitali mapema sana tukawa tumekaa kusubiri wauguzi na madaktari waje kwa ajili ya kutupa huduma lakini tuliona kila nesi ama daktari akija wanaenda kujikusanya sehemu moja tukadhani kuwa wana jambo lao wanajadili lakini ilipofika saa tatu asubuhi ilitubidi tukawaulize inakuaje mbona huduma hatupati ndipo wakatuambia hali ya usalama katika kazi yao siyo nzuri kwani kuna baadhi ya wagonjwa wanawatishia amani, ’’alisema Janet.
Baada ya kutokea kwa taharuki hiyo Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga alifika katika hospitali hiyo na kuzungumza na wagonjwa pamoja na wauguzi ili kuweka mambo sawa ili huduma zianze kutolewa kama kawaida.
‘’Kweli tumesikiliza pande zote kuhusiana na suala hili na hatupo hapa kwa ajili ya kupendelea mtu suala la kuhudumia wagonjwa ni wajibu wa kila muuguzi na daktari, wagonjwa ndiyo wateja wenu hivyo hali ya usalama tunalifanyia kazi na hakutatokea vurugu zozote.
“Mimi ndiye mkuu wa ulinzi na usalama hapa wilayani, nitahakikisha kuwa usalama unaimarika kila wakati ili mweze kufanya kazi yenu vizuri na wananchi wapate huduma zinazostahiki,” alisema Konisaga kisha huduma zikarejea.