MPANGO wa kumuua Catarina ili kuwamaliza kabisa mashahidi ambao wangeweza kusimama mahakamani na kutoa ushahidi dhidi ya bilionea Jackson Motown umekamilika, amechukuliwa na Padri Colonel, kutoka kwenye nyumba alimofichwa na FBI na kupelekwa kwenye kilima cha New York Mountain Top.
Ajali ya kutengeneza inaandaliwa kwa gari alilokwenda nalo kugongeshwa kwenye katapila, kisha Ofisa wa FBI, Clarence aliyekuwa akishirikiana na wauaji kuuawa mbele ya macho yake! Hilo lilipotendeka ndipo Catarina alikamatwa na kulazwa chini, akashangaa kumuona Padri Colonel akinyanyua nyundo kubwa kwa ajili ya kumpiga nayo kichwani, hapo ndipo akafahamu kumbe hakuwa padri bali ni muuaji wa Jackson Motown; Dracula.
Hayo yakitokea, upande mwingine, mtu aliyeaminika kwamba ni marehemu; Kevin amepatikana! Thomas Edmund ndiye aliyefanya mpango wa kumuondoa ndani ya nyumba yake ya shambani na kwenda kumficha kwenye nyumba yake ya mjini New York, wakawa wanampatia dawa za usingizi na kumlisha kwa kutumia dripu, yote hayo ni kuhakikisha kuwa haiingii mikononi mwa Jackson Motown ambaye pia Thomas Edmund alimchukia.
Je, nini kitaendelea?
SONGA NAYO…
“…AND where is Catarina?” (Catarina yuko wapi?) aliuliza Kevin, Bwana na Bibi Edmund wakaangaliana, hawakuwa na jibu la kumpa.
“Catarina?” Thomas Edmund aliuliza akionyesha mshangao.
“Yes.” (Ndiyo)
“I really don’t know where she is!” (Kwa hakika sijui mahali alipo!)
“She disappeared before Jackson Motown captured me!” (Alipotea kabla Jackson Motown hajaniteka!)
“No! I saw at your funeral!” (Hapana! Nilimuona kwenye mazishi yako!)
“So she is somewhere alive!” (Kwa hiyo yuko hai mahali fulani!)
“I guess!” (Nafikiri)
“I want to meet her, she is my wife to be, I came to America for only one thing; Catarina!” (Nataka kukutana naye, ni mke wangu mtarajiwa, nilikuja Marekani kufuata kitu kimoja tu; Catarina!)
“But at the moment you can’t leave the house, Jackson Motown will kill you!” (Lakini kwa sasa huwezi kuondoka nyumbani, Jackson Motown atakuua!)
“I am not scared of death any more, death should be scared of me!” (Siogopi kifo, kifo ndiyo kinatakiwa kiniogope mimi!)
“That’s why we kept you on sedatives; we knew you would leave this house forcefully!” (Hiyo ndiyo sababu tulikuwa tunakupa dawa za usingizi kila siku, tulijua ulitaka kuondoka hapa nyumbani kwa nguvu!)
Waliendelea kumtuliza na kumsihi awe mvumilivu mpaka hali itakapotulia ndipo aondoke nyumbani kwao kwenda kuendelea na kazi ya kumtafuta Catarina, Kevin akakubaliana nao, hata hivyo hakutaka kufahamu nini kilikuwa kikiendelea katika maisha ya Jackson Motown, akiweka wazi kabisa kwamba ndiye binadamu aliyemchukia kuliko wote.
“His murder and rape cases are still in court, unfortunately there are no witnesses to prove that he raped and murdered people!” (Kesi zake za kubaka na mauaji bado ziko mahakamani, bahati mbaya sana hakuna mashahidi wa kuthibitisha kwamba alibaka na kuua watu!)
“I’m the witness!” (Mimi ni shahidi!)
“Can you stand in court?” (Unaweza kusimama mahakamani?)
“Why not?” (Kwa nini nisisimame?)
***
Watu wote walioshirikiana na Dracula kulitengeneza tukio la ajali ya Catarina ambalo lilitikisa Jiji la New York na Marekani nzima, sababu lilimhusisha pia ofisa wa FBI na kupotea kwa Padri Colonel pamoja na Catarina, walikutwa wamekufa ndani ya nyumba waliyoishi, uchunguzi wa polisi ulipofanyika ilithibitika kuwa jiko la mkaa walilokuwa nalo chumbani walimolala kujiongezea joto ndilo lililowaua kwa kutoa moshi wenye sumu ya iitwayo carbon-monoxide.
Hakuna mtu aliyefahamu kilichotokea nyuma ya tukio hilo, Dracula ambaye wakati huo alishayatupa mavazi ya kipadri na kubaki katika hali yake ya kawaida ndiye aliyeucheza mchezo huo, akahakikisha kabisa kuwa hakuna mtu yeyote zaidi ya yeye na Jackson Motown waliofahamu kilichokuwa kikiendelea!
Catarina hakujulikana alikokwenda, wazazi wake walikuwa wamechanganyikiwa kabisa, kwani walikuwa na uhakika gari lililopata ajali ndilo lililombeba kutoka kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi pamoja. FBI walikuwa katika msako mkali wa kumtafuta Padri Colonel ambaye waliamini huko alikokuwa lazima alikuwa na Catarina, haikuwa rahisi kumhusisha Dracula na Padri Colonel, alikuwa mitaani akiendesha maisha yake na kuwashangaa watu waliokuwa wakimtafuta.
Vifo vya watu hao pamoja na Catarina vilimfurahisha sana Jackson Motown, sasa alikuwa na amani kwani kusingekuwa na mtu mwingine yeyote wa kutoa ushahidi dhidi yake, alipokutana na Dracula gerezani alipofika kumtembelea baada ya kazi hiyo kukamilika, alimpongeza na kuahidi kumlipa kitita kikubwa cha Dola ambacho katika maisha yake yote asingekisahau.
“Thank you so much!” (Asante sana!) Dracula alishukuru.
“You have done a good job, I cannot imagine how would life be without you!” (Umefanya kazi nzuri, nashindwa kuelewa maisha yangekuwaje bila wewe!)
“You are very important person to me!” (Wewe ni mtu muhimu sana kwangu!)
“Thank you, these cases are over now, I’m going to be out of here next week!” (Asante, hizi kesi sasa zimefika mwisho, nitakuwa nimetoka humu wiki ijayo!)
“How comes your sight is back?” (Inakuaje uwezo wako wa kuona umerejea?)
“I wasn’t blind, I just faked it to fool the police!” (Sikuwa kipofu, nilijifanya tu ili kuwatapeli polisi!)
****
Alichokisema Jackson Motown ndicho kilichotokea, kesi yake ilianza kuendeshwa kila siku, upande wa mashitaka ulipotakiwa kuleta mashahidi, hakuna aliyepatikana! Mahakama ikalazimika kumuachia Jackson Motown huru, yeye na Dracula wakaondoka kifua mbele hadi nyumbani ambako wawili tu walifanya sherehe ya kunywa mvinyo kufurahia ushindi, saa tatu usiku, Jackson Motown alimtaka Dracula amfuate ili akamlipe ujira wake.
Wakashuka hadi ufukweni, nyumba ya Motown ilijengwa kandokando kabisa ya bahari, wakaingia ndani ya boti ambayo Motown aliiwasha mara moja ikaitika, ndipo wakaanza kukatisha maji wakielekea katikati ya Bahari ya Atlantic, nusu saa baadaye, Jackson Motown alizimisha boti, akachomoa bastola kiunoni na kumwamuru Dracula asimame akiwa amenyoosha mikono juu.
“It is time for the killer to be killed, so that everything can remain a secret!” (Ni wakati wa muuaji kuuawa, ili kila kitu kibakie siri!)
“What?” (Nini?) Dracula aliuliza akishangaa.
“I have to kill you Dracula!” (Inabidi nikuue Dracula!)
“You can’t do tha…!” (Huwezi kufanya hivy…” ) hakuweza kumalizia sentensi yake, milio ya “Paaaa! Paaaa! Paaaa!” ikasikika, Dracula akadondoka ndani ya boti na kutulia, alichokifanya Motown ni kuchukua kamba na kuifunga kwenye chuma kizito kilichokuwa ndani ya boti yake, kisha kuufunga mwili wa Dracula kwa kamba ile.
Akauchukua mwili huo na kuuzamisha majini kisha akakichukua chuma kilichofungwa kwenye kamba, kikamfuata ndani ya maji, akacheka akiamini Dracula asingeonekana tena duniani.
Je, nini kitafuata? Dracula amekufa? Catarina yuko wapi? Alikufa? Fuatilia hadithi hii katika Gazeti la Championi Jumamosi.
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO===>https://www.facebook.com/shigongotz/
KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA TUFOLLOW
INSTAGRAM===>https://www.instagram.com/globalpublishers/
TWITTER===>https://twitter.com/GlobalHabari
FACEBOOK===>https://www.facebook.com/GlobalPublishers
YOU TUBE===>https://www.youtube.com/user/uwazi1