×

Baraka Da Prince ampoza Linex

barakaBarakah Da Prince

Nyemo Chilongani

Mwanamuziki anayekuja kwa kasi kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Barakah Da Prince ameamua kumpoza mwanamuziki mwenzake, Sunday Mjeda ‘Linex’ baada ya stori kuenea mitandaoni kwamba alivunja amri ya sita na mchumba  wa Linex mara baada ya picha iliyomuonesha msichana huyo akiwa na mwanaume aliyefanana na Barakah.

Linex-Sunday Mjeda ‘Linex’

Akichonga na gazeti hili kwa njia ya simu Barakah alisema kwamba mara ya kwanza alipozisikia stori hizo, alishtushwa nazo kwani anamheshimu sana Linex na hawezi kufanya hivyo kutokana kuwa na ukaribu naye na hata huyo mwanaume, amefanana naye tu na si yeye.

“Nilishtushwa nilipozipata stori hizo. Siwezi kufanya upuuzi huo, namheshimu Linex, mwanaume yule si mimi, labda tumefanana tu. Najiheshimu na hata huyo msichana simfahamu kabisa,” alisema Barakah.

Leave a Comment