Stori: Francis Godwin, Ijumaa
NJOMBE: INASIKITISHA! Sylvester Mgowolwa, mkazi wa Kijiji cha Bulongwa, wilayani Makete mkoani Njombe, amejinyonga baada ya kudaiwa kumnyonga mchumba wake hadi kumuua.
Kahimu RPC Njombe, SSP JohnTemu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo hivi karibuni ambapo amesema marehemu alifikia uamuzi huo baada ya kutofautiana na mchumba wake.
Kamanda Temu alisema marehemu ameacha ujumbe kwamba sababu ya kujiua na kumuua mpenzi wake ni kwa kuwa alimsomesha chuo cha u-nesi, akamfungulia duka la dawa baridi na kumjengea nyumba ya kuishi mjini Njombe kisha akaanza visa.
Mgowolwa alisema mpenzi wake huyo alibadilika ambapo waliishi kwenye mgogoro mkubwa yeye akaamua kuomba kuachana naye lakini kwa kugawana mali ambazo alimnunulia kitendo hicho mpenzi wake alikikaataa ndipo akaamua kuchukua uamuzi huo.