ILIPOISHIA RISASI JUMATANO:
“Jamila, tuondoke tafadhali,” alisema baba Rehema. Nikatingisha kichwa kukubaliana naye kisha akasema tena…
“Lakini wewe siwezi kukupeleka nyumbani moja kwa moja, lazima ukapumzike kwanza mahali, sawa?” pia nikamkubalia kwa kutingisha kichwa.
JIACHIE MWENYEWE SASA…
Baba Rehema alinibeba hadi kwenye kituo cha teksi, akakodisha. Nilimsikia akisema…
“Suka please, nipeleke kwenye gesti yoyote ile?”
Halafu nikamsikia huyo suka akisema…
“Gesti au hospitali mkuu?”
Baba Rehema alisisitiza gesti, safari ikaanza. Nililala siti ya nyuma nikiwa nahisi nimelala miguu juu, kichwa chini. Nilijilazimisha sana kuinua kichwa ili nione ulalaji wangu lakini nikashindwa. Baada ya muda nikasikia gari imesimama, baba Rehema akauliza…
“Inakuwa shing’ ngapi?”
“Elfu tatu tu kaka.”
Ukapita ukimya, mara baba Rehema akanitoa, akanibeba mpaka ndani ya gesti, nikamsikia mtu, mwanamke akiuliza:
“Huyu unamleta humu ili kufanya nini badala ya hospitali?”
“Haumwi,” alijibu baba Rehema.
“Kama haumwi mbona umembeba?”
“Amelewa.”
“Hee! Kulewa gani huko jamani! Mpaka unabebwa!” yule mwanamke alisema.
“Si unajua tena!” alisema baba Rehema.
Alipewa chumba, akaniingiza ndani na kunilaza kitandani kisha akanivua mavazi na yeye pia, akanibeba tena mpaka bafuni ambako aliniogesha kwa tabutabu.
Baada ya maji kugusa mwili wangu nikabadilika, nikapata nguvu na kuweza kusimama mwenyewe, nikatembea mwenyewe mpaka chumbani na kujifuta maji na taulo.
“Jamila,” aliniita…
“Abee…”
“Kumbe pombe huziwezi?”
“Sirudii tena baba Rehema. Kumbe ndivyo zilivyo!”
Baba Rehema alinicheka, akasema eti nisijali, tukianza mchezo tu, baada ya kumaliza pombe yote kichwani itakwisha…
“Kweli baba Rehema?” nilimuuliza nikiwa siamini…
“We utaona tu.”
Tulitulia kidogo wote, tukaangaliana kwa muda, mimi nikajikuta naachia tabasamu mwenyewe, baba Rehema akanisimamisha, akanikumbatia na kunipapasa mpaka mwenyewe nikaenda kitandani, akaja. Tuliingia uwanjani..!!!
***
Sasa tukawa tunaongea zetu huku tumelala. Mara simu ya baba Rehema iliita…
“Sijui atakuwa nani?” aliuliza akiifuata…
“Mama Rehema, usiongee kwanza nimalizane naye,” baba Rehema alisema akapokea…
“Haloo…nini..? Saluni gani..? Haa! Sasa kwa masaa mawili hayo ndiyo unakuwa na wasiwasi mama Rehema?! Labda kama ungeniambie aliondoka toka asubuhi…kwani we hujui saluni kuna foleni? Baadaye bwana, kama hatarudi mpaka giza tutajua la kufanya,” baba Rehema akakata simu huku akicheka…
“Teh! Teh! Teh! Teh! Bosi wako kaingia mchecheto huko, anajua umetorokea kwa mabwana…”
“Ni kweli, si nimetokea kwako,” nilimtania baba Rehema.
Baada ya kupita kama saa moja hivi, kweli nilirudi katika hali yangu ya kawaida.
“Baba Rehema si tuondoke sasa,” nilimwambia…
“Hamna, yaani lazima tucheze tena ndipo tuondoke,” alisema baba Rehema huku akinishikashika sehemu mbalimbali za mwili, si nikapagawa bwana!
Kazi ikaanza tena, safari hii afadhali maana hatukuchukua zile dakika arobaini za mchezo, tukamaliza kila kitu…
“Sasa tunaweza kuondoka baby,” baba Rehema alianiambia baada ya kutoka kuoga wote.
“Sawa.”
Kwenye kutoka sasa, baba Rehema akaniambia aanze yeye halafu akishafika nje na kuangalia mazingira, atanipigia ili na mimi nitoke, nikakubaliana naye.
Alipotoka, ndani ya dakika moja tu, mlango ukasukumwa kwa nguvu, mwanamke akaingia ndani…
“Ahaa! Unajua nimeogopa sana kumwona yule baba anatoka peke yake halafu wewe umo ndani na uliingia kwa kubebwa,” aliniambia akiwa amesimama mlangoni.
“Niko sawa sasa, na mimi pia natoka muda si mrefu,” nilimwambia, akaondoka zake.
Mara simu iliita, nikasimama na kuanza kutoka huku naipokea…
“Nakuja…nakuja,” nilimwambia baba Rehema, akakata simu.
Tulipanga mimi ndiyo nitangulie kurudi nyumbani lakini nimwambie mama foleni ilikuwa kubwa na muda unakwenda hivyo nimeshindwa kusubiri, nitarudi kesho yake.
Nilikuta geti kubwa limefungwa, ikabidi nigonge kwa nguvu, nikasikia tembea ya mama akija getini…
“Wewe nani?” aliuliza kwa ukali…
“Mimi Jamila mama.”
“Jamila gani na wa wapi?”
Nilishangaa sana kuulizwa hivyo…
“Mimi Jamila mfanyakazi wako wa ndani mama, nilikuaga nakwenda saluni kutengeneza nywele.”
Je, unajua nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi Jumatano ijayo.