Wiki iliyopita nilianza kuwachambulia tabia ambazo mwanamke akiwanazo lazima mwanaume amkimbie, leo nitahitimisha ‘topiki’ hiyo kwa tabia zilizosalia ambazo ni zifuatazo;
KULINGANISHA
Hii nayo ni tabia isiyopendwa na wanaume wengi. Wanaume wanapenda kuishi maisha yao. Wanapenda kuheshimiwa na wapenzi wao. Wanapenda kumsikia mwanamke akisema; ‘hakuna mwanaume mwingine wa kufanana na wewe.’
Mwanaume anapenda kuhakikishiwa kwamba hakuna mwanaume mwingine kama yeye. Yeye ndiye mzuri au bora kuliko wanaume wengine hivyo mwanamke anapoanza kuonesha tabia za kumlimnganisha na
mwanaume mwingine linakuwa tatizo kubwa.
.
Mwanaume anakasirika. Anaona ni rahisi mwanamke wake kumtamani mtu mwingine baki kuliko yeye. Sifa anazozitoa kwa mwanaume mwingine ni nzuri hivyo zinamvutia. Kama zinamvutia siku yoyote anaweza kushawishika kumfuata yule anayemvutia.
KUWA TEGEMEZI
Wakati mwingine hata kama huna kitu lakini mwanamke unashauriwa kutojionesha una kitu. Jioneshe
kwamba una kitu hata kama huna. Wanaume wa sasa hawapendi kuwa na
mwanamke tegemezi wa kila kitu.
Hata kama huna kazi ni vyema mwanamke afanye biashara ndogondogo zitakazompunguzia mwanaume wake makali ya kuombwa fedha kila wakati jambo ambalo likizidi huwa kero kwao. Mwanaume akigundua mwanamke ni tegemezi katika hatua za mwanzoni ni rahisi kumkimbia na kwenda kwa mwanamke ambaye angalau atakuwa hamtegemei kwa kila kitu.
WASIO WAELEWA
Mwanaume anapenda mwanamke muelewa. Hapendi mwanamke mbishi. Anatamani kuwa na mwanamke ambaye akimueleza kitu, anajiongeza na kufanya zaidi ya pale mwanaume alipofikiria. Mwanaume anapenda mwanamke atakayeanzisha wazo la kimaendeleo na kumshirikisha mpenzi wake ili walifanye kinyume chaku humkimbia.
KUJITAPA KWA KUWA NACHO
Hakuna mwanaume anayependa kutawaliwa. Wanawake wenye fedha mara nyingi wanakuwa na tabia ya kutaka kuwatawala wanaume. Anatumia fedha zake kama fimbo ya kumchapia mpenzi wake. Ni vigumu sana wanaume kumvumilia mwanamke wa aina hiyo, mara nyingi wanajiepusha naye. Kwa kutumia fedha zake anaweza kupata mwanaume mwingine lakini pia watashindwana katika suala la kumtawala.
KUWA BIZE SANA
Wanaume wengi hawapendi mwanamke tegemezi lakini pia wanaume haohao wanachukia mwanamke akiwa bize sana na kazi zake. Mwanaume hapendi kuona mwenzi wake anakuwa bize na kazi au biashara zake kiasi ambacho kitamfanya hata akose muda wa kuwa pamoja.
Unachotakiwa kufanya hapo mwanamke ni kujigawa. Hakikisha unakuwa bize na kazi lakini si ya kupitiliza maana itamfanya mwanaume akose muda wa kuwa na wewe pale anapokuhitaji, badala yake anaweza kwenda kwa mwanamke mwingine ambaye hayupo bize.
Niwatakie siku njema, tukutane wiki ijayo kwa darasa lingine la kusisimua!