Ezekia Wenje akiwa Mahakamani
Mamia ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe leo wamefurika kwenye eneo la Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza katika kesi ya mbunge wa zamani wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA) anayepinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba mwaka jana yaliyompa ushindi wa ubunge wa jimbo hilo, Stanslaus Mabula (CCM).
Polisi wametumia nguvu ya ziada kuhakikisha ulinzi unaimarika mahakamani hapo.
Mbunge wa Nyamagana Staslaus Mabula akiwa mahakamani
Ezekiel Wenje akisubiri kutoa ushahidi
Freeman Mbowe na Ezekiel Wenje wakiwa mahakamani.