×

Kisa Mtonyo, muonekano na madawa… mastaa hawa wapukutika

JAPO linatokea lakini Kibongobongo linaweza lisiwe jambo la kawaida msanii hasa wa kiume kujipunguza kwa kiasi kikubwa uzito wa mwili wake na kubadilika kabisa.
Kwa mbele jambo hili limekuwa likitokea mara kwa mara kwa mastaa kupungua ghafla miili yao ‘kupukutika’ aidha kutokana na mtonyo, muonekano ama kutumia madawa ya kulevya kupitiliza.
Ukweli ni kwamba listi ya mastaa hao ni ndefu, lakini katika makala haya inawaanika baadhi ya mastaa wa ndani na nje ya nchi ambao walipukutika kwa sababu fulani, baadaye wakarudia katika hali zao za kawaida lakini wengine wakapata mabadiliko ya kudumu.

50 Cent
Rapa huyu kutoka Marekani anasifika kwa kuwa na mwili wa kuvutia uliojengeka kimazoezi.
50 aliuacha ulimwengu mdomo wazi mwaka 2010 alipokuwa kwenye maandalizi ya kuigiza baadhi ya vipande ndani ya Filamu ya Things Fall Apart, akiwa mgonjwa aliyeathirika kwa saratani ambapo alilazimika kupungua uzito kutoka kilogram 97 hadi 72 kwa muda wa wiki tisa.
Njia hasa aliyoitumia rapa huyu kupunguza mwili wake ilikuwa ni kuweka utaratibu maalum wa mlo wake, lakini zaidi alipata ushauri wa kidaktari ambapo baada ya muvi kumalizika 50 Cent alirudia katika hali yake ya kawaida.

Rick Ross
William Roberts II ‘Rick Ross’ ambaye pia ni bosi wa Maybach Music Group, miaka ya hivi karibuni naye alilazimika kujipunguza uzito kutokana na kuchukizwa na muonekano wake.
Rapa huyo mwenye sauti nzito, mwaka 2014 alikuwa na kilo zisizopungua 136 lakini baada ya kuamua kuupunguza mwili wake huo kwa muda wa miezi saba tu alikuwa amepunguza kilo 45 na kubakiwa na 91.
Akifanya mazungumzo na mitandao mbalimbali ya burudani nchini Marekani rapa huyo alisema aliamua kujipunguza mwili wake kutokana na kutopendezwa nao ambapo alilazimika kujikita zaidi kwenye ulaji wa matunda pamoja na maji mengi, basi!

Baghdad
Novemba 2, 2013, rapa aliyefahamika zaidi kupitia ngoma ya Full Ng’aeng’ae na Kundi la Mexcana  La Cavela, Baghdad alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Katika sherehe hiyo Baghdad alipewa zawadi mbalimbali huku moja ya zawadi hizo ilikuwa ikimtaka kubadili muonekano wake huku na kusisitiza kuimarisha afya yake iliyokuwa imeyumba kutokana na maradhi ya kisukari.
Kwa mujibu wake, Baghdad amewahi kusema kuwa baada ya kuupokea ujumbe huo aliamua kuufanyia kazi kwa kwenda kuonana na wataalam wa afya ambao walimpa dozi maalum ya vidonge ambavyo alitakiwa kuvitumia kwa muda wa miezi mitatu.
Wakati anaanza kuitumia dozi ya dawa hizo, Baghdad alikuwa na uzito unaofikia kilo 149 lakini baada ya kutumia kwa muda wa miezi hiyo iliyokuwa imepangwa uzito wake uliporomoka mpaka kilo 100.

Christian Bale
Huyu ni muigizaji maarufu duniani na mshindi wa Tuzo ya Oscar mwaka 2011 kupitia Filamu ya The Fighter, aliyeigiza akiwa muigizaji mkuu msaidizi (Supporting Character). Staa huyu anaingia kwenye listi hii baada ya mwaka 2004 kupunguza uzito kutoka kilo 90 hadi kufikia kilo 27 na kufanikiwa ‘kufit’ kwenye nafasi aliyotakiwa kucheza katika Filamu ya The Machinist.

Rob Kardashian
Mwanamitindo huyu ambaye ni kaka wa Mwanamitindo na Mtangazaji, Kim Kardashian, baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na tatizo la uzito kuwa mkubwa amefanikiwa kuupunguza.

Kevin wa Home Alone
Staa huyu kijana aliyewahi kujizolea sifa baada ya kubamba na Filamu za Home Alone naye ni miongoni mwa mastaa waliopukutika kutoka miili yao ya awali

Leave a Comment