×

Nay amchana Dudubaya

Nyemo Chilongani
MSANII anayetamba na ngoma ya Shika Adabu Yako, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amemchana mwanamuziki mkongwe, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’  kwamba asijilinganishe na yeye kwani muziki anaofanya, maisha anayoishi ni tofauti kabisa.

Akizungumza kupitia kipindi kimoja cha televisheni, Nay alisema amemsikia Dudabaya kwenye televisheni akisema staili ya kuwachana watu anayoitumia Nay ameikopi kutoka kwake.

“Dudabaya asijilinganishe na mimi, yeye alipenda ugomvi kwa kuamini ungemuweka juu kimuziki ndiyo maana aligombana na wanamuziki wenzake, mimi nakuchana kwenye mistari ila mtaani sina fujo, sipigani na mtu, sasa akitaka kujilinganisha na mimi, anakosea,” alisema Nay.

Leave a Comment