Inakuwaje masela wangu wenyewe? Kitaa hii haina kwere ni fulu mzuksi aisee arifu kwani inakuwa nini? Basi sawa kama vepe sogea kwa fasi hii mjanja wako ndo kama hivo nipo kwa mahewa mazee.
Ebana mbishe za kusaka mabovu si zinasonga? Kama vepe tuendelee kukaza kozi hakuna kusanda hadi kieleweke jamaa yangu. Mwanangu Kima ananing’ata sikio kwamba duniani kinachopendwa ni mkwanja na kazi ya moyo ni kusukuma damu siyo kupenda.
Huku na huku baba la baba nipo na chama langu la ukwehe chobingo, nagonga mdudu nusu na ndizi mbili si ndo msela na shori wake wakakinukisha? Mazee asikwambie kichwa palichimbika hatare wanangu.
Eti msela wangu ametoka auti na mpango wa kando kitu cha hawara dheni wanazinguana kisa foni tu. Yaani hata auti yenyewe haikunoga kabisa kozi ilikuwa ni mwendo wa kuuchubua mwanzo mwisho hadi wakaamua kusepa hata sinyaki picha huko mbele ya safari nini kilihapeni.
Oya kachaa unaambiwa wakati makaksi hao wanatimba kiotani kwa ajili ya bata ndefu walikuwa wanapetiana na kuitana bebi kwa sana, yaani fulu mzuksi bati kiliponuka kila mmoko alikuwa kavimba ileile. Si unajua zile staili za kiloko za kuchuniana?
Basi bana, baada ya kutimba kiwanja, msela na kitu chake komfotabo akaagiza mdudu kilo moko, ndizi bee za shori na ugali mmoko wa mwanangu mwenyewe.
Wakati wakisubiria madikodiko kutoka kwa bwaashee si ndo jamaa akaanza kugombea foni ya shori kwa madai kuwa alikuwa anachati na mwana mwingine! Ebana unaambiwa palikuwa hapatoshi mbaya kozi mbebiz alitia ngumu jamaa kushika simu yake bati mwishoni ilibidi asande tu akaisalimisha kwa msela. Jamaa alipocheki si ndo akagundua shori anachati na chuma kingine? Ilikuwa noma usipime. Hivi wana mnanyaka talaka ya hawara? Achana na mangumi na masumbwi kozi unaweza ukakata mtu kitu cha pumzi dheni ukaozea lupango. Kwa infomesheni yako talaka ya hawara ni kibuti tu dheni bizinesi iishie hapo.
Unaambiwa hata msosi ulipotimba kwa fasi ya mezani hakukuwa na mbwembwe wala kulishana kama wengine walivyokuwa wanafanya.
Hadi mwisho wa mpango mzima pipo walitimua eneo la tukio wakiwa wamenuniana ile kiroho mbaya aisee chalii yangu.
Mmenisoma mabibi na mabwana? Kama vepe nduki, sii yuu neksti wiki.