Staa wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan ‘Tiko’.
Na Hamida Hassan
Staa wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan ‘Tiko’ amesema anatamani sana kuchora tatuu mwilini mwake ila kinachompa hofu ni maelezo kuwa wanaofanya hivyo wapo hatarini kupata kansa ya ngozi inayoweza kuwasababishia kifo.
Akipiga stori na Ijumaa Tiko alisema kila akimuona mtu amechora tatuu anavutiwa naye lakini kwake inamuwia ngumu kufanya hivyo.
“Kwanza kujichora tatuu hasa kwa sisi watoto wa Kiislam ni dhambi, sasa ukiwa umejichora ile ambayo haifutiki kisha ukafariki sijui utamwambiaje Mungu wako.
“Lakini pia, tatuu zinaelezwa kuwa zinasababisha kansa ya ngozi, kwa maana hiyo nikijichora nijue kuna hayo madhara, sasa ya nini nijitafutie kifo wakati bado natamani kuishi?” alihoji Tiko.