×

Steve anaswa kashikilia ‘zigo’ la Wellu

Na Musa Mateja
Msanii wa filamu anayeheshimika Bongo Muvi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ juzikati alinaswa akiwa amemshikilia kimahaba msanii mwenzake, Wellu Sengo jambo lililoibua minong’ono.
Tukio hilo lilinaswa na paparazi wetu kwenye pati iliyoandaliwa na waigizaji ili kumpongeza Mheshimiwa Paul Makonda kwa kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Wakati watu wakiwa kwenye mishemishe za kupiga picha na mheshimiwa huyo, Steve alionekana akiwa bize na mdada huyo aliyefungashia ambapo alimshika zigo lake huku Wellu naye akipitisha mikono yake mabegani mwa mshikaji huyo.
Haikuweza kufahamika kama kuna kinachoendelea kati ya wawili hao au ni upendo wa kawaida tu licha ya huko nyuma kuwahi kudaiwa wana kaukaribu f’lani amaizing.

Leave a Comment