×

Huyu Naye…Fuata Maelekezo-12

ILIPOISHIA RISASI JUMATANO:
Mimi sijui nini kilitokea mwenzenu, lakini nilijikuta nikipayuka bila kujali kama nitasikika au la huko nje lakini huku mlango wa chumbani kwangu nao ukigongwa kwa nguvu…
“Ngo ngo ngoooo!”
TAMBAA NAYO MWENYEWE…

“Mh!” niliguna, nikajua mama Rehema amerudi tena, nikakata sauti ya kupayuka kwangu.
Nilibaki kimya, baba Rehema alishatoka uwanjani, akawa upande wa ukutani. Hakuna aliysema neno mpaka hapo. Ukimya ulitawala…
“We dada Jamila,” aliita Rehema…
“Ah! Kumbe Rehema bwana,” baba yake alisema…
“We! Isijekuwa amekuja na mama yake halafu wewe unasema kumbe Rehema bwana,” nilimwambia baba Rehema akaonesha kuelewa.
Nilitoka kitandani polepole nikihakikisha kitanda hakipigi kelele na kwenda kufungua mlango…
“Unasemaje Rehema?” nilimuuliza huku nikijifunga kanga vizuri baada ya kumwona Rehema yuko peke yake…
“Mlango wa chooni haufunguki huko!”
“Kivipi?”
“Nafungua hautaki kufunguka, mimi nataka kwenda chooni,” alisema Rehema huku akipigapiga miguu chini kuashiria kwamba, alibanwa!
Nilirudi chumbani kukiwa giza, nikamwambia baba ‘ake…
“Rehema anasema mlango wa chooni umegoma kufunguka nakwenda kumfungulia.”
“Sawa,” tuliongea kwa sauti ya chini sana.
Moyoni niliamini niko sahihi kwa yote niliyokuwa nikiyafanya, sikujua kwamba najichimba shimo kubwa mimi mwenyewe.
Baada ya kumfungulia mlango Rehema ambao mimi binafsi sikuona huko kugoma kwake, nilirudi ndani chumbani kwangu kama vile mtu anayekwenda kwa mume wake.
Nilijitupa kitandani na kudakwa na baba Rehema…
“Si unajua tulikatisha,” alisema baba Rehema huku akianza kunimiliki licha ya kwamba kulikuwa na giza.
Tuliingia tena uwanjani, mpira ukachezwa kwa kiwango cha hali juu mpaka dakika tisini zote ambapo kila mmoja alitoka uwanjani kwa sare sare.
“Mpenzi wangu,” nilimuita baba Rehema naye akaitikia kama mimi nilivyoita…
“Nenda kwako sasa, muda umekwenda.”
“Nitakwenda,” alinijibu kwa mkato.
Hali yake ilionesha kwamba, hakuwa anataka kwenda kwa mkewe jambo ambalo kwangu lilinishangaza sana tena sana…
“Mbona kama hutaki kwenda kwako?” nilimuuliza.
“Nitakwenda.”
“Lini?”
“Muda si mrefu. Halafu naomba acha kuniuliza maswali hayo mimi siyataki. Kwani mimi sijui kwamba kule ni kwangu? Acha mambo yako bwana,” kama alikuja juu f’lani hivi.
Mwishowe kwa kujivuta saaana, baba Rehema alitoka kitandani kwangu na kuvaa, akaondoka zake.

***
Huku nyuma, nilianza kuwaza…
“Hivi huyu baba Rehema ina maana amedhamiria kabisa kuwa na mimi au? Kwangu anapata nini zaidi kinachomfanya amuone mkewe kama kunguru wa mwitu?
“Au mapigo yangu makubwa? Ina maana mkewe hayawezi haya au naye ndiyo vile tena hajibidishi kwa sababu ya ule mwili wa kulakula?”

***
Kulikucha, mimi hausigeli kawaida yangu ilikuwa ni kuamka saa kumi na moja alfajiri ya kila siku na kuanza usafi wa chooni, bafuni kisha sehemu nyingine ili wao wakiamka wakute chooni kunakanyagika.
Mama Rehema alifuata baadaye kabisa akaja kunikuta jikoni tena alikuja kama kwa kunyata wakati ninavyomjua tembea yake ni kama anacheza ngoma, pata…pata…pata..!
“Jamila,” aliniita…
“Abee mama, shikamoo…”
“Hapana, achana na shikamoo yako. Nataka uniambie ukweli wako Jamila, usinifiche hata kitu kimoja…wewe unatembea na mume wangu baba Rehema? Usinifiche.”
“Siyo kweli,” nilimjibu kwa mkato sana.
“Ni kweli.”
“Anika ushahidi wako hapa sasa hivi,” nilimwambia kwa sauti ya kujiamini sana.
“Upi zaidi ya huo unaoujua wewe moyoni mwako,” aliniambia kwa sauti ya umbeya…
“Wa moyoni mwangu mimi ni upi? Mbona we mama Rehema hujiheshimu kama wamama wengine. Kama unahisi mume wako anavutiwa na mimi si mnitimue kazi tu ijulikane moja mama!”
“Jamila…Jamila…leo hii unafikia hatua ya kuniambia mimi sijiheshimu siyo? Kwa hiyo mimi nina akili kama za Rehema?”
“Rehema amekuzidi mama,” nilimwambia huku nikiendelea na kazi za jikoni.
Nilishtukia niko chini, miguu yake ikinikanyaga kama vile amekanyaga kapanya kalikokuwa kakileta tabu ndani ya nyumba…
“Baba Rehemaaa,” niliita kwa sauti ya juu.

Je, unajua nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi Jumatano ijayo.

Leave a Comment