×

Ajali ya Basi Yaua 6 Iringa

ajaliWATU 6 wamekufa na  wengine  38 kujeruhiwa  vibaya  baada  ya  basi lenye  namba  za  usajili    T 798 AKV mali ya Lupondije Express linalofanya safari za  Mwanza kwenda  Iringa  kupinduka  eneo la  Mteremko  wa Ipogolo  mjini  Iringa.

Mashuhuda wanasema kuwa basi hilo lililotakiwa kumalizia safari yake mjini Iringa lilipitiliza kwenda Ipogolo kwa minajiri ya kufaulisha abiria wachache wa Mbeya. Imeelezwa   kuwa baadhi ya  abiria    waliokufa  katika  ajali   hiyo na  majeruhi   ni  wale ambao   walitakiwa   kumaliza safari yao mkoani Iringa lakini dereva  wa basi  hilo aligoma   kuwashusha  na  kupitiliza kwenda Ipogolo    kufaulisha abiria  wa Mbeya  kwanza  ndipo arudi   kuwashusha  wa Iringa.

12920532_1094739447256715_3223310280829406857_nAjali   hiyo  imetokea  majira ya  saa 2 usiku jana baada ya  basi  hilo  kufeli  breki katika  mteremko  huo huo mkali kabla ya  kupinduka katika eneo linalojulikana kama Kisima cha Bibi.

Wema  Zuberi  ni  mmoja kati ya majeruhi  wa ajali  hiyo aliyekuwa ametoka mkoani  Dodoma  kuelekea  Mbeya  alieleza kuwa  mwendo  wa  basi hilo  haukuwa  mkali  bali kawaida.

Majeruhi huyo alieleza kuwa   baada ya  kuingia katikati ya  mji  wa Iringa ndipo dereva  wa basi   hilo alionesha  kuendesha basi   hilo kwa mwendo mkali  zaidi  kiasi  cha  baadhi ya  abiria  kulalamika mwendo huo na  kutaka   kushushwa ila dereva  hakuwasikiliza zaidi ya  abiria  hao.

“Abiria  wengi   walionyesha   kumlalamikia   dereva   huyo kwanza  kutokana na  kuwapitiliza  stendi pasipo  kuwashusha na pili mwendo  kasi ambao  alikuwa  akienda nao   ili  kufanikisha  kutufaulisha abiria  tuliokuwa   tukielekea  Mbeya” alieleza

Zaidi alisema, kabla ya  kufika  eneo  hilo ambalo  basi  lilipinduka kuna kona kali na mteremko  mkali  na kilichoonekana haraka  haraka ni  dereva   kushindwa kukata  kona   hiyo baada ya Breki  kufeli   na   hivyo  kulazimika  kuhama  njia  na  kugonga kingo za  barabara  hiyo na  kupinduka .

Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  Bw  Richard Kasesela akizungumza na  mwandishi  wa  habari  hizi eneo la   tukio alisema  kuwa zoezi la  kuendelea  kutafuta  miili  iliyobanwa na basi  hilo imekuwa  ngumu  kutokana na kukosekana  kwa gari la kuinua  basi hilo na  tayari  amemwagiza  meneja  wa Tanesco kuleta  gari  hilo na  iwapo  dereva   hayupo  basi

Hata   hivyo  alisema  kuwa kuanzia   sasa  dawa  ya  madereva  hao  ni  kuwashughulikia kwani kama Rai imekwisha   tolewa  mara  nyingi na  bado  ajali  zinaendelea   kutokea.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa aliahidi  kutoa  taarifa mara  tu zoezi hilo  litakapokamilika kwa kuinua  basi hilo na kutazama kwa  kina kama kuna  miili ambayo  imefunikwa   chini ama la.

Mwandishi  wa habari  hizi  alishuhudia  miili  minne ikiwa tayari  imetolewa katika basi hilo huku majeruhi   wengi  wakiwa   wamepata majeraha  makubwa  mikononi ,miguuni na kichwani,Majeruhi  wa ajali   hiyo wamelazwa Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa  wa Iringa.

Leave a Comment