Khadija Kopa (Kulia) na wasanii wake wakiserebuka.
Wanamuziki wa East Africa Melody wakiimba kwa pamoja.
Mwanahidi Shabani wa East Africa akiimba.
Sofia Mohamedi wa Ogopa Kopa nae akitoa burudani.
Jagwa akionyesha umahili wake wa kuimba na kucheza.
Jagwa akiserebuka.
Msagasumu nae akiwapelekesha puta mashabiki.

Na Issa Mnally
SIKUKUU ya Pasaka ilinoga jana kwenye Ukumbi wa Taifa wa burudani wa Dar Live, Mbagala Zakhiem- Dar baada ya mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani zilizokuwa zikipamba moto ukumbini hapo.
Usiku huo ulikuwa wa aina yake kutokana na vikundi vya Mchiriku na Taarabu kutoana jasho kiasi cha kuwafanya mashabiki kuwa na hamasa na kuserebuka vya kutosha huku amshaamsha na shangwe zikitamba.
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY)
