×

Huyu Naye..! Fuata Maelekezo-13

ILIPOISHIA GAZETI LA RISASI JUMAMOSI:
“Rehema amekuzidi mama,” nilimwambia huku nikiendelea na kazi za jikoni.
Nilishtukia niko chini, miguu yake ikinikanyaga kama vile amekanyaga kapanya kalikokuwa kakileta tabu ndani ya nyumba…
“Baba Rehemaaa,” niliita kwa sauti ya juu.
SASA KAZANA NAYO MWENYEWE…

Unamwita huyo kwa sababu ni bwana‘ako siyo?” alisema mama Rehema huku nikimsikia baba Rehema anakuja…
“Kuna nini Jamila?”
Baba Rehema aliuliza kabla hajaingia jikoni, aliponikuta mimi niko chini na mguu wa mke wake upo juu yangu, akamzaba kofi moja mama Rehema…
“Muuaji mkubwa wewe, ndiyo nini hivi?” aliuliza baba Rehema wakati mkewe yupo chini anagalagala kwa lile kofi moja tu…
“Tatizo nini?” aliuliza tena baba Rehema…
“Unamtetea kwa sababu ni bibi yako siyo? Mimi sikubali nitakula sahani moja na yeye. Lazima nikuue Jamila,” mama Rehema aliniahidi kwa sauti iliyojaa hasira.
Mumewe alimuuliza kama ana wasiwasi na mimi kuwa natembea naye, kwa nini asimuulize yeye badala ya kuniuliza mimi? Pia alimwambia kwamba, anaponipiga anajua historia yangu? Je, kama nina ugonjwa wa kifafa?
“Sasa sikia mama Rehema, sasa hivi fungasha kila kilicho chako ondoka kwangu. Mimi na mwanamke mgomvi mbalimbali kabisa.”
“Naondoka ndiyo,” alisema mama Rehema akisimama na kwenda chumbani kwake.
Mimi nilijua utani lakini baada ya muda, nikamwona akitoka na mabegi matatu ya nguo…
“Mbaki salama, mle maisha vizuri,” alisema huku Rehema akilia…
“Wee…weee! Usinitibue Rehema…nakwambia kabisa usinitibue, baki hapahapa na baba yako malaya mkubwa,” alisema mama Rehema akifunga mlango kwa kuubamiza.
Japokuwa yeye ni mtu mzima, mimi msichana, lakini kauli aliyoitumia kwa mtoto wake siyo! Huwezi kumwambia mtoto wenu kwamba baba yake malaya, huko ni kumkuza katika maadili ya kutokuwa na adabu katika jamii.
Basi, mama Rehema aliondoka kweli katika mazingira hayo na siku hiyo Rehema hakwenda shule kutokana na mtafaruku huo. Hata baba Rehema hakwenda kazini.
Tulikuwa nyumbani tu, nyumba ilipoa kama vile kuna msiba. Ingawa wakati f’lani baba Rehema alijitahidi kwa kuweka CD ya nyimbo za Bongo Fleva na kufuatisha wanavyoimba.

M
chana, baba Rehema hakula, lakini Rehema alikifyeka chakula vizuri sana huku akiangalia katuni kwenye tivii. Alishasahau kuondoka kwa mama yake mzazi.
Baada ya chakula cha jioni ambacho siku hiyo tulikila saa kumi na mbili badala ya saa moja au moja na nusu, baba Rehema alisema anakwenda kulala zake.
Rehema naye aliingia chumbani kwake mapema sana, sebuleni nikabaki mimi peke yangu. Sasa nikawa najiuliza, je kuondoka kwa mama Rehema kumevunja penzi langu na baba Rehema? Mbona hanitumii meseji?
Nikaanza mimi…

Mpenzi wangu umelala?”
Muda huohuo nikapata majibu…
“Sijalala mpenzi, ili nilale ni lazima niwe na wewe, hivi hapa nilitaka kukutumia meseji uje chumbani tulale.”
Baada ya kusoma meseji hiyo ya baba Rehema, palepale siyo kwamba niliamka, bali nilikurupuka, nikatupa rimoti huko, nikazima swichi ukutani, nikatoka hadi chumbani kwa baba Rehema.
Tangu nimeanza kazi kwenye nyumba hiyo, siku hiyo ilikuwa ni mara yangu ya pili kuingia kwenye chumba hicho.
“Lakini ngoja nikaoge kwanza,” nilimwambia baba Rehema huku nikimwangalia kwa macho yaliyojaa shauku ya kuwa na yeye.
Niliamini kwamba, katika mazingira yale, ilikuwa ni lazima nikaoge. Nilitoka, nikaenda chumbani kwangu, nikajifunga kanga moja tu, nikaenda kuoga.
Nikiwa naoga nilianza kuyaona maisha katika mwanga mwingine. Kwangu yalikuwa maisha maangavu, nikaamini kuwa, niko njiani kama siyo kukaribia kufika, kuolewa na baba Rehema au kuwa mke wa baba Rehema…
“Rehema atakuwa ananiita mama mdogo atake asitake. Kwanza kuanzia kesho nitamwambia awe ananiita mama mdogo,” nilijisemea moyoni mwangu.
***
Nilipanda kitandani kwa baba Rehema nikiwa na kanga yenye majimaji kwa mbali baada ya kutoka kuoga. Wakati napanda, baba Rehema alinidaka kama kichaa aliyekuta jalala lenye vyakula vibovu…
“Sweetheart wangu huyo,” alisema huku akinikaribisha na busu moja tu lakini zito…
“Chwaaa!” mpaka nikajishika kwenye shavu utadhani nimelipukiwa na bomu la kutengeneza kwa mkono.
Niliitoa ile kanga na kuitupilia kwa mbali, nikabaki mimi kama mimi tu! Nikaona bado, nikamchojoa baba Rehema. Na yeye akabaki yeye kama yeye tu…

Twende kazini baba,” nilimwambia baba Rehema.
Kwani na yeye alisubiri? Aa wapi! Kwanza mnara ulikuwa unasachi sawasawa mawimbi ya sauti.
Ilikuwa hekaheka shuka kuchomoka kwenye kitanda. Ilionekana yeye ana hasira za mke wake kuondoka na mimi nina hasira za kuondokewa na bosi wangu wa kike. Lakini pia ilionekana yeye ana furaha ya kuwa na uhuru na mimi na mimi nilikuwa na furaha ya kukaribia kuitwa mama mdogo na Rehema.
Sehemu gani ya kitanda ambayo usiku huo hatukufika? Kona zote tulimaliza, wakati fulani tukahamia nje ya kitanda na huko ndiko nilikoanza kuuliza mustakabali wangu…
“Mpenzi?”
“Yes!”
“Sasa mimi nitakuwa mke mdogo au mpango huo wa kuwa na mke baada ya mama Rehema kuondoka haunao…wewe niambia tu, mimi nitapokea yote lakini naomba sana nijue mwisho wangu kwako ndani ya nyumba hii,” nilifunguka.
Sasa sikiliza majibu yake…
Je, unajua nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi Jumamosi ijayo

Leave a Comment