ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
“Rozimina…we Rozimina,” kaka Cheni alimuita, hakuitika…
“Sista unajua atakuja kusema kweli kwa baba…”
“Aseme, ana ushahidi gani?”
“Si vile ulivyomjibu…”
“Ah! Aende zake huko.”
Mara, tukamwona Rozimina anarudi akiwa ameshikiliwa mkono na mama…
JIACHIE MWENYEWE SASA…
“
We Cheni, huyu Rozimina analia nini?” mama alimuuliza kaka Cheni, mimi mapigo ya moyo yakapanda…
“Hata mimi sijui mama, kaja hapa analia, akaondoka analia.”
Rozimina alibaki ameduwaa tu kwani alijua kuwa, akisema linalomliza angeuharibu ukoo wetu. Alijua mama asingekaa kimya kusikia mimi binti yake natoka na kaka yangu wa damu. Nilianza kujuta kumjibu Rozimina vile.
Nilionesha dalili zote za upole maana Rozimina kila wakati alikuwa akiniangalia mimi kwa macho makali na ya kunisuta…
“Au mama amekupiga nyumbani?” mama alimuuliza Rozimina…
“Hata…”
“Sasa nini?”
“Au Cheni amekufokea?”
“Hata.”
Labda niseme kidogo kwamba, katika wanawake wa kaka Cheni, sijui kwa nini Rozimina alikuwa akimkubali sana, sijui kwa nini!
“Basi nenda nyumbani kapumzike,” mama alimshauri Rozimina.
Nilimwona Rozimina akiondoka huku akiniangalia mimi zaidi kuliko kaka Cheni na kuliko mama…
“Mbona unamwangalia sana huyu? Eti wewe mbona anakuangalia sana, umemfanya nini?” mama alituuliza wote…
“Mimi sijamfanya lolote mama ila labda kama yeye ana kero yake kwangu. Lakini si umeshauri aende akapumzike. Rozimina nenda tu,” nilisema nikamshika mkono na kutoka naye.
Moyoni nilijutia sana kitendo changu cha kumjibu Rozimina vile kwamba mimi na kaka Cheni asituingilie. Maumivu yake yalikuwa hapo akizingatia sisi ni ndugu wa damu moja…
“Rozimina, mimi na kaka Cheni hatuna uhusiano wowote. Kunikuta nimevaa kanga moja tu wala si ishu. Niliingia kwake kumpa funguo za chumbani kwa mama maana mimi nataka kwenda kuoga ili nitoke na mama alienda msibani, usinifikirie vibaya Rozimina,” nilimwambia. Ndiyo kwa mbaaali nikamwona kama ananielewa, akaachia na tabasamu…
“Lakini wifi hata ungekuwa wewe usingenielewa mfano uje nyumbani halafu unikute katika mazingira tata na kaka Johnson halafu nikujibu vibaya.”
“Nimekuelewa Rozimina,” nilimkubalia kwa sauti ya ‘yaishe basi jamani!’
Hapo tulikuwa mbali na nyumbani na kilichotokea, Rozimina aliondoka akiwa na furaha tele na mimi nikarudi nyumbani nikiwa na furaha.
Nilimkuta mama anatoka tena…
“Wewe uangalie nyumba. Sisi haturudi leo, nilikuja kuchukua hela tu aliniagiza baba yako. Nimefurahi sana wanangu nimewakuta mpo nyumbani wote. Kuzurura hakufai wanangu jamani muwe mnasikiaga!”
“Sawa sisi tumekuelewa sana. Kwanza nimegundua sijui kwa nini nilikuwa mtembezi wakati naweza kutulia hapahapa nyumbani mama ‘angu,” alisema kaka Cheni.
Mimi moyoni nilisema…
“Mama mngejua, mngeturuhusu tu kwenda kuzurura, yanayofanyika hapa nyumbani mama ni makubwa sana. Usijeshangaa mimi nabeba mimba hapahapa.”
“Na wewe unasemaje? Kaka yako ametambua makosa yake na baba yake nitakwenda kumwambia kwamba Cheni amebadilika, nimemkuta nyumbani. Wewe je?” mama aliniuliza mimi…
“Mama hata mimi kama kaka Cheni. Kwanza unajua mama mimi si mzururaji sana kama alivyo kaka Cheni…”
“Siyo kama nilivyo, kama nilivyokuwa,” kaka Cheni alidakia hata kabla mimi sijamaliza…
“Ee…kama ulivyokuwa zamani. Kwa hiyo hata mimi mama sitakiwi kuwa msichana wa kutokatoka.”
“Nimefurahi sana wanangu, mlale salama. Ila kesho mchana we Cheni uje kuzika.”
“Sawa mama.”
Mama alipoondoka tu, kaka Cheni akanifuata, akanikumbatia kwa nguvu na kunipiga busu akisema…
“Mke wanguuuuu…”
“Niambie mume wangu,” na mimi nilisema hivyo.
Usiku uliingia, nikapika, kaka Cheni alikaa kwenye kiti anachopenda kukaa baba wakati akisubiria chakula. Eti tulijifanya mimi mama, yeye baba…
“We mama Cheni,” aliita kaka Cheni…
“Abee mume wangu…”
“Hicho chakula bado tu jamani?”
“Baba Cheni sasa hivi unakula.”
“Harakisheni bwana, njaa inauma sana, mchana sikula.”
“Sawa baba Cheni.”
***
Tulimaliza kula, kila mmoja alikwenda kuoga tukaweka mjadala kwamba, wapi tunalala usiku huo. Chumbani kwa kaka Cheni au chumbani kwangu…
“Mimi nataka chumbani kwako kaka Cheni. Kitanda chako hakipigi kelele kama changu,” nilitoa wazo na sababu…
“Hapana, tulale kwako. Dirisha lako kubwa hewa inaingia, si unajua shughuli ya leo ni nzito kuliko zote. Kwa mara ya kwanza tunalala wote mpaka kesho asubuhi.”
Tulikubaliana kulala kotekote. Chumbani kwa kaka Cheni kwa sababu kitanda chake hakipigi kelele mpaka saa sita usiku halafu kuanzia hapo tunaingia chumbani kwangu mpaka asubuhi maana dirisha ni kubwa linaingiza hewa vizuri.
Tulipanda kitandani kwa kaka Cheni. Tulikuwa tunavuta kasi ya msisimko kwanza, nje dirishani kwake tukasikia mtu amekanyaga bati likatoa mlio.
Je, nini kiliendelea? Usikose kusoma wiki ijayo.