×

Oya masela gunia tupu halisimami!

Makachaa na maduu wangu niaje…ni vepe? Wooza! Kipande hii ni shwari ileile. Ndo kama hivo mtu mzima nimeshatimba kwa fasi ya jamvini kukinukisha. Ebana mambo ya holidei ya kitu cha Pasaka si yalikuwa yechuyechu kwenye mstari machalii? Dah! Wanangu siyo mzuksi wala nini hata hakuna kukaribishana mazee? Acheni roho mbaya masela wangu.

Oyo chama langu, pamoko na kitu cha mnuso kwenda biyee bati si unanyaka tena mizinguo huwa haikosekani? Mazee unaambiwa wana wametumbua mzigo wote hapa tunapochati wana wapo apache alolo. Hapa chezea viti virefu wewe!

Hivi wanangu mnanyaka kuwa mshumaa hauwezi kuwaka wenyewe bila kuwashwa? Basi bana huku na huku mshua na mkidi wake wa miaka bee si akatimba tauni Bongo tambarare kutoka mkoa? Pamoko na ishu zingine bati alitaka na famili yake nayo ionje japo kidogo utamu wa jiji la maraha na karaha.

Basi ile anatinga tu Ubungo akaona achukukue kabisa kitu cha rumu kwa fasi ya gesti moko femasi kitaa hiyo ya Ubungo ili iwe simpo kufanya mishemishe na famili.
Mazee walipotimba tu ndani ya rumu, hapo ndo pana bonge la mkasa yaani fulu kwere kozi kilichohapeni ni noma sana arifu.

Mshua anakuteli kuwa ile anazama tu kwa rumu na mai waifu na mkidi wake wa kiume, akawasha taa dheni akaenda kwenye swichi ya kitu cha tiivii. Dooh! Kucheki kilichokwenda kwa mahewa ilikuwa ni picha za kiutu uzima tena jamaa wako katikati ya mechi, watoto wa mbwa wanaita pilau.

Ebana ilikuwa soo kozi mshua alikuwa anahaha kutafuta rimoti ili achenji chaneli bati hakuiona hadi alipopata maindi ya kuzima kwenye swichi. Pamoko na jitihada hizo bati tayari mkidi alikuwa ametupia kitu cha jicho na kujionea laivu bila chenga aisee chaliiangu.

Sasa imajini ungekuwa parenti ungemteli vepe mkidi akusome? Watu wazima wanakwambia gunia tupu halisimami so kama mshua akawa anajitahidi kupotezea na kuweka mambo freshi. Basi bana lawama zote zikadondoka kwa maweita na mawetiresi wa gesti.

Masela hii ishu inaonekana kuwa komoni kinoma bati kuna vichwa vingine huwa havimaindishi kabisa kuona maishu ya dizaini hiyo kozi kinachowapeleka pale ni kuresti na kumbonji na siyo mambo fekelo. Unanyaka vichwa vingine kama mimi ni viongozi wa dini so kama vipi ni beta pipo wakazipotezea ili kutowazingua wana wasiomaindisha vitu kaa hizo.

Mmenisoma wanangu wenyewe? Kama vipi tuwachane dheni laifu limuvu fowadi

Leave a Comment