
Masoud Kipanya (wa kwanza kushoto), Fina Mango (wa pili kulia) na Fredwaa wakiwa katika pozi leo ndani ya studio za Clouds FM.

Mtangazaji Fina Mango akipitia magazeti wakati wa kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na Clouds FM leo.
WATANGAZAJI wa zamani wa Clouds FM, Masoud Kipanya na Fina Mango wamerejea rasmi kwenye kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na Clouds FM.
Watangazaji hao wameanza kusikika leo asubuhi ‘live’ wakiwa pamoja na Babra Hassan na Fredwaa.
Uwepo wa watangazaji hao wa zamani, umekuja siku moja baada ya watangazaji wakongwe wawali wa redio hiyo kudaiwa kuitema ambao ni Gerald Hando na Paul James ‘PJ’.